Teknolojia mpya kutumika Barclays Premier League
Posted in
No comments
Saturday, July 7, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Teknolojia ya kuthibitisha kama mpira umevuka msitari na kuingia wavuni, inayofahamika kama 'Goal-line technology',
huenda ikatumiwa katikati ya msimu wa ligi kuu ya Premier ya England,
ya mwaka 2012 hadi 2013, baada ya utaalamu huo kuidhinishwa na
halmashauri ya kimataifa ya mchezo wa kandanda, IFAB, Alhamisi, mjini
Zurich.
Teknolojia mbili ziliidhinishwa, moja ikifahamika kama 'Hawk-Eye', yaani 'jicho la mwewe', na ya pili inafahamika kama 'GoalRef', ikimaanisha 'mwamuzi wa goli'.
Teknolojia
hiyo kwa mara ya kwanza itatumiwa katika michuano ya Kombe la Dunia la
vilabu vya soka mwezi Desemba, na iwapo itaonekana inafaa, basi
itatumiwa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho mwaka 2013, na vile
vile katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.
Mbinu hiyo ya 'jicho la mwewe' inafanya kazi vipi?
Utaalamu huu unategemea kamera sita, zikiangazia kila lango, na kuufuata mpira uwanjani.
Kisha kiufundi, huwa teknolojia inatambua mahali halisi mpira ulipo, kupitia utaalamu unaojulikana kama 'triangulation'.
Ikiwa mpira utavuka msitari wa goli, basi ujumbe
kupitia mawimbi ya redio hutumwa moja kwa moja hadi katika saa ya
mkononi aliyovalia mwamuzi, kumwarifu kwamba bao limefungwa.
Kama kanuni za FIFA zinavyohitaji, utaratibu mzima hauchukui zaidi ya sekunde moja.
Teknolojia ya 'GoalRef' nayo hutumia kifaa kinachojulikana kama 'microchip', ambacho hubandikwa katika mpira unaotumiwa, na kwa kutumia mawimbi ya smaku karibu na goli.
Iwapo mabadiliko funali yatajitokeza katika
mawimbi kupitia mpira kuvuka msitari, teknolojia inaamua kama hilo ni
goli, na kisha kwa njia ya elektroniki, mwamuzi hujulishwa katika muda
wa sekunde moja kwamba goli limefungwa.
Wasimamizi wa ligi kuu ya Premier wamesema wanataka kuanza kuitumia teknolojia hiyo mpya haraka iwezekanavyo.
Katika mkuu wa chama cha soka cha England, Alex
Horne, amesema ni wajibu wa wasimamizi wa ligi kuu ya Premier kuamua ni
lini wangelipenda kuanza kuitumia teknolojia hiyo mpya.
"Tayari tuna teknolojia ya Hawk-Eye
katika uwanja wa Wembley, kile kinachohitajika tu ni kuiweka sawa na
kuhakikisha inafanya kazi vizuri na kuidhinishwa kwa leseni, na kwa hiyo
tumekaribia sana kukamilisha matayarisho yetu katika kuitumia
teknolojia hiyo.
"Kombe la FA huenda likatufanyia uamuzi, kwa
kuwa tunaweza kuitumia katika nusu faianli na fainali za FA, na sidhani
huo ni uamuzi ambao utata."
Horne aliongezea kwamba anahisi "hii ni siku muhimu sana" kwa kandanda.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :