JK AIPA VYOMBO VIPYA VYA MUZIKI VIJANA JAZZ
Posted in
No comments
Saturday, December 15, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Wana wa
Vijana Jazz wakiwa kazini, Kulia ni, Saburi Athumani (Kiongozi wa
bendi), Abdallah Mgona Hazelu (Katibu wa bendi), Nuru Mhina 'Baby Whiye'
na Roshi Mselela, wakiimba ukumbi wa Masae Bar, Kawe.
***
NA BASHIR NKOROMO.
BAADA ya
kuwa 'juu ya mawe' kwa muda mrefu, bendi ya muziki wa dansi ya Vijana
Jazz, ' Wana Air pambamoto' imeibuka upya kuanza kupiga muziki kwenye
kumbi za starehe, huku ikiwa imeipua vibao viwili vipya kusuuza nyoyo
za mashaki wake.
Ikipiga
kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa Masae Bar, Kawe wilaya ya Kinodoni
jijini Dar es salaam, usiku wa kuamkia leo, bendi hiyo imedhihirisha
kwamba mashabiki wake wengi bado wapo.
Kwenye
ukumbi huo unaotazamana na kilichokuwa kiwanda cha kusindika nyama cha
Tanganyika Packes, Vijana Jazz ilithihirisha kuwa 'bado wamo', kwa
kupiga nyimbo zake za zamani zikiwemo 'Mary Maria', 'Mwsiho wa mwezi',
'Ngapulila' na 'mawifi', zilizopigwa enzi za muasisi wa bendi hiyo,
marehemu Ahmed Maneti katika miaka ya 1980.
Nyimbo
hizo ziliwafanya mashabiki wa bendi hiyo, kucheza kwa hamasa kubwa huku
baadhi yao wakifuatisha kuimba sambamba na wanamuziki waliovyokuwa
wakiimba jukwaani na wengine kwenda jukwaani kutuza waimbaji.
Licha ya
kuonyesha kuwa bendi hiyo bado ni mahiri, wanamuziki wa zamani iliobaki
nao ni Roshi Mselela, Nuru Mhina (Baby White) na viongozi wa bendi
Abdallah Mgonahazelu (Katibu) na Saburi Athuman ambaye ni kiongozi wa
bendi.
Vibao
vibya ambavyo bendi hiyo imeipua ni 'Utanieleza nini', utunzi wake
kiongozi huyo na Kina mama wanaweza uliotungwa na Mgonahazelu.
Athumani
alisema, nyimbo hizo zimesharekodiwa na hivi karibuni zitaanza kuingizwa
sokoni, lakini akasema bendi yake itafanya hivyo baada ya kuzipiga mara
nyingi majukwaani na kuzoeleka masikioni kwa mashabiki wao.
Alisema
wakati kazi ya kuzirekodi nyimbo hizo kwa ajili ya kiusikilizwa,
imeshakamilika, sasa bendi imo katika jitihada za kuzirekodi katika
video ili ziweze kurushwa kwenye vipindi vya Televisheni na pia kuuzwa
kwa mashabiki.
"Tunamshukuru
Rais Jakaya Kikwete ametutoa juu ya mawe, hivi vyombo mnavyoona
ametuwezesha mheshimiwa Kikweye. Kwa kweli tunamshukuru sana", alisema
Mgoma Hazeru wakati kabla ya bendi hiyo kuanza kuimba wimbo wao mpya wa
'Utanieleza nini'.
Vijana
Jazz ni moja ya bendi ambazo Mratibu wa Budurani zote kwenye ukumbi huo
wa Masae, Juma Mbizo, amesema atakuwa anazitumia kutoa burudani kwa
mashabiki. Nyingine ni kama Msondo Band na FM Academia 'Wazee wa
Ngwasuma'.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :