MAANDALIZI YA PAMBANO LA CHEKA NA CHIMWEMWE YAIVA
Posted in
No comments
Saturday, December 15, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
MAANDALIZI la pambano la
Francis Cheka na bondia Chiotka Chimwemwe toka Malawi litakalochezwa
Desemba 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Abeid Amani Karume jijini
Arusha yamekamilika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam promota wa pambano hilo Andrew George amesema taratibu za mchezo huo umekamilika.
"Taratibu zote za pambano zimekamilika kwa asilimia 90 ikiwa pamoja na kumtumia tiketi bondia Chiotka Chimwemwe", alisema George.
George alisema ameamua kulipeka pambano hilo Arusha kwa kuwa anaamini watu wa Arusha wanapenda ngumi na siku hiyo ni siku ya sikukuu hivyo watakuja kwa wingi pamoja na familia zao kwani pambano litaanza saa nane mchana.
Pia alisema mabondia watapima uzito siku ya sikukuu ya krismasi jijini Arusha.
Pambano hili litakuwa ni la raundi 12 na Mmalawi huyu anajigamba atampiga Cheka ndani ya ardhi ya nchi yake hivyo kuwasihi watanzania kuja kwa wingi kwani hata ulinzi utakuwepo wa kutosha, alisema George.

MOJA YA MABANGO YALIYOTAPAKAA JIJINI ARUSHA KWA SASA KUHUSU MPAMBANO HUO. |
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :