Maandalizi Chaga Day yapamba moto

Posted in
No comments
Friday, December 14, 2012 By danielmjema.blogspot.com

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAANDALIZI ya kufanyika kwa tamasha la Wachaga yanaendelea vizuri, kwa ajili ya kuhitimisha kwake Desemba 22 mwaka huu katika viwanja vya Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro kuanzia saa 4:00 asubuhi, ikiwa ni siku tatu kabla ya Sikukuu ya Krismasi.

Akizungumza na Handeni Kwetu jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment
Paul Mganga, alisema tamasha hilo linalenga kuhamasisha jamii  juu ya  utamaduni wa kabila hilo na mengineyo nchini.

Vilevile, kuhamasisha jamii na familia zao zilizopo ndani na nje ya mikoa yao kukumbuka nyumbani na kutembelea wazee mara kwa mara.

“Tuna imani kubwa kuwa zaidi ya watu 3,000 na familia zao, watahudhuria kwa wingi tamasha hili la kihistoria huku wakipata fursa ya kusikia historia ya  kabila  la Wachagga kwa kina toka kwa wazee wanatoka kwenye familia za Machifu naMangi Mkuu wa kabila hilo wanaoishi mkoani Kilimanjaro.

“Kuona na kucheza ngoma zote za asili za kichaga pamoja na vikundi tofauti tofauti vya ngoma za asili na sanaa za makabila mengine,” alisema.

Kadhalika kutakuwa na vyakula  vya asili  vya aina zote kama kiburu, kisusio, mtori, ndafu, shiro, kiumbo, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande na vingine vingi.
 
Pia vinywaji vyote vya asili vya kabila hilo kama mbege, dadii  na  vingine vingi.

Mganga alitaja burudani mbalimbali zitakazokuwepo siku hiyo kuwa ni bendi ya Akudo Impact, Msanii Mfalme Costa Siboka kutoka Dar es Salaam na wasanii wote kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha watapamba tamasha hilo.

Katika tamasha hilo viongozi mbalimbali wa serikali wamealikwa pia , wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro, viongozi wa asasi zisizo za kiserikali pamoja na asasi za serikali yetu, wakurugenzi wa makampuni ya utalii na hoteli kubwa za mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Mganga alisema wamejipanga vizuri katika kufanikisha siku za makabila yote Tanzania kila mwaka tukianza na makabila wa kaskazini, lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kuenzi mila na tamaduni za makabila yetu na kukumbuka kuzipeleka familia zetu nyumbani tuwapo nje ya mikoa yetu.

Tamasha la  Chagga Day  limedhaminiwa na Safari Lager, Pepsi, Konyagi, Precision Air, Radio 5 FM, Toyo, Samsung, Michuzi Blogspot, Zizou Fashion, Mlonge Bi Makai, Egesha Trading Agency, CXC Africa, Delina Group Enterprises, Linda Media Solution (LIMSO) and Albert Msando Legal Consultant. Kiingilio ni sh.5,000 mlangoni.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .