WATUHUMIWA WA UTAPELI WA FEDHA WATIWA MBARONI
Posted in
No comments
Friday, December 14, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
RPC KILIMANJARO-ROBATH BOAZ |
JESHI la Polisi Mkoani Kilimanjaro, linawashikilia watu sita,
wakazi wa Moshi mjini, ambao wanasadikika
kuhusika na kundi kubwa la Matapeli ambalo limekuwa likiwasumbua wakazi wa Moshi,
kwa muda mrefu sasa kwa matukio ya utapeli ambayo yameshamiri mjini
hapa kwa muda mrefu sasa.
Watuhumiwa hao walikamatwa jana katika maeneo ya Boma Ng’ombe,
wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro baada ya wananchi kutoa taarifa ya uwepo wao
katika kituo kidogo cha polisi cha Boma Ng’ombe wakiwa na vifaa vyao vya
utapeli.
Kundi hilo limekuwa likisakwa na Jeshi la Polisi kwa muda
mrefu ambapo inadaiwa kuwa wamekuwa wakiwatapeli watu kwa kuwadanganya wananchi
watu kuwa wanauwezo wa kuwatengezea fedha nyingi kwa kutumia mitambo yao.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa Polisi
mkoani Kilimanjaro, Robath Boaz alisema watu waliokamatwa ni Athumani Ally
(39), ambaye anadaiwa kuwa ni mganga wa kienyeji , Emanuel Jacob (20),
Christian Samwel (23), Jolvin Joseph (26), Aziza Athumani (26) na mtu mmoja
mwenye asili ya kihindu ambaye anadhaniwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo
Kasim Somji (31).
Kamanda Boaz alisema kuwa watu hao kwa sasa wanashikiliwa na
jeshi la polisi na kuongeza kwamba uchunguzi unaendelea kuwasaka wanachama
wengine wa mtandao huo na mara tu uchunguzi utakapomalizika watafikishwa
mahakamani.
“Kwa sasa watuhumiwa wote wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
na mara tu baada ya kumaliza uchunguzi sheria itafuata mkondo wake,” alisema
Kamanda Boaz.
Wakati huohuo Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro
linamshikilia, mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Wasiwasi John (28), ambaye ni mmakonde, mkazi wa Pasua
Matindigani, kwa tuhuma za kukutwa na Noti bandia.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku
akiwa anajaribu kutumia noti hizo bandia, zenye namba za usajili BC 2937831 na
BK 3153543 kufanya manunuzi dukani.
Kamanda Boaz, alisema kuwa mtu huyo atafikishwa mahakamani
mara tu baada ya uchunguzi kukamilika na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana
na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa inapotokea kuna kundi lolote la watu
wanawashuku au kubaini jaribio lolote la utapeli na uhalifu.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :