Wakenya kuchezesha Stars na Zambia

Posted in
No comments
Friday, December 14, 2012 By danielmjema.blogspot.com


 Msemaji wa TFF, Boniface Wambura

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limesema kuwa mwamuzi Sylvester Kirwa, kutoka Kenya, amepangwa kuchezesha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Handeni Kwetu jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema mwamuzi huyo anatambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mwamuzi huyo atasaidiwa na Elias Wamalwa na Marwa Range, huku waamuzi hao wasaidizi ambao vilevile watatoka Kenya pia wanatambuliwa na FIFA.

“Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini hoteli ya Tansoma, na inafanya mazoezi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake,” alisema Wambura.

Mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka, ikiwa ni siku chache baada ya timu ya Taifa, Kilimanjaro Stars, kushindwa kufanya vizuri katika michuano ya Chalenji, iliyomalizika nchini Uganda.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .