MH. DKT. HUVISA AZINDUA TAARIFA YA HALI YA MAZINGIRA YA JIJI LA DAR ES SALAAM LEO.
Posted in
No comments
Tuesday, December 18, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais –
Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa
Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema
katika Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN)
uliofanyika mjini Kampala Julai 2002, ulibaini kuwa ukosefu wa taarifa
za hali ya mazingira katika bara la Afrika ni moja ya sababu
zinazochangia mipango duni ya usimamizi wa shughuli za maendeleo na
utekelezaji Mikataba ya Kimataifa ya utunzaji mazingira.
Amesema kutokana na hali hiyo AMCEN
iliiomba UNEP wafadhili program ya Afrika ya Mtandao wa Hali ya
Mazingira (Africa Environmental Information Network) ili kuongeza uwezo
wa nchi za Afrika wa kuwa na Taarifa za Hali ya Mazingira na Mtandao wa
Habari baina ya nchi za Afrika.
Mh. Huvisa ameweka wazi kuwa taarifa hiyo
imekamilika na iko tayari kwa ajili ya utekelezaji, na kuwa taarifa
hiyo imeezea Historia ya jiji la Dar es Salaam, Jiografia na Fiziolojia
yake, suala la uchumi Jamii, Sera, Sheria na Mfumo wa Utawala
Kimazingira, Usimamizi wa Rasilimali ya Ardhi, Rasilimali Maji, Madini
na Nishati, Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira, Uchafuzi wa
Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi. (Picha zote na Mo Blog).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.
Sazi Salula akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es
Salaam akisema Tanzania ni moja ya nchi zinazotekeleza program ya
mtandao wa taarifa za hali ya mazingira yaani “Africa Environmental
Information Network (AEIN) chini ya ufadhili wa Shirika la Mpango wa
Mazingira Duniani (UNEP).
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini
Tanzania Phillipe Poinsot akizungumza kabla Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa hajazindua Taarifa ya
Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema taarifa hiyo
ina mapendekezo makuu 12 na kutoa wito kwa serikali ya Tanzania
kutafakari kila pendekezo sambamba na kuzitumia taarifa za kimazingira
kwa manufaa ya taifa.
Afisa Mwakilishi wa UNEP Tanzania
Clara Makenya akizungumza machache kabla ya kuzinduliwa kwa Taarifa ya
Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam na kusisitiza kuwa UNEP
inatambua umuhimu wa kuwa na ripoti kama hiyo, hivyo amewataka wahusika
kuipitia na kuielewa kwa makini na utekelezaji wa yalimo uanze kwa muda
muafaka.
Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Abdallah Chaurembo akitoa neno la shukrani kwa wafadhili wa
Programu ya Mazingira wakati hafla ya uzinduzi wa taarifa ya hali ya
Mazingira ya jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akikata utepe kuzindua rasmi
taarifa ya hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam. Wanaoshuhudia
tukio hilo ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (kushoto) Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Phillipe Poinsot (wa tatu kulia), Afisa
Mwakilishi wa UNEP Tanzania Clara Makenya (wa pili kulia) na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava ( wa kwanza
kulia).
Sasa imezinduliwa rasmi.
Pichani Juu na Chini ni Maafisa Kutoka
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wakurugenzi, wawakilishi wa vyombo
vya habari , Wakurugenzi wa Manispaa za jiji na Wadau wa Mazingira
waliohudhuria halfa ya uzinduzi wa taarifa hiyo.
Mgeni rasmi Dkt. Therezya Huvisa akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa UNEP/UNDP pamoja na wadau wa Mazingira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Phillipe Poinsot pamoja na Afisa
Mwakilishi wa UNEP Tanzania Clara Makenya baada ya uzinduzi taarifa ya
hali ya mazingira ya jiji la Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa
chuo cha Taifa cha Utalii jijini Dar leo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :