Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300
walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho,
aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea
Uganda miaka michache tu.
Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana
majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli
zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana
kwa siri.
Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao
wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari,
na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa
waasi wanaotafuta makaazi.
Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar
na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa
alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911.
Baada ya
udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za
mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja.
Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho
kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka
1963.
Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha
bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji
wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.
Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963
ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha
kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja).
A.S.P (Chama
cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya
wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu
lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo
lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa
Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.
Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni
matukio ya kawaida siku hizo. Nakumbuka nilikuwa naendesha baskeli
kuelekea shuleni kupitia makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina
mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara
vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza.
Vikundi mbali bmali
vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya
fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa,
Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi
ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni
ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.
John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini
alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa
nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.
Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa
vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi.
Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha
kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda?
Jee,
wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo
halali? Au kama alivyotaraji,
wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono?
Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya
hivyo? John Okello alichezesha dadu
usiku huo wa mwezi wa Januari.
Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi
wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi.
Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa
na shuku ya kukata fundo hilo gumu
la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala.
Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao.
Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani.
Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.
Baadhi ya
viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo
kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi
hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa
"Mapinduzi".
Makundi
ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria
na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.
Walimiliki ardhi
na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na
mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa
kweli mji wenyewe uliporwa.
Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyengine waliuliwa kwa makundi.
Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine
baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.
John
Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani
zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na
Pemba.
John Okello alitangaza
vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga
yeye. John Okello aliamini alikuwa
akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa
kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza
ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi…
ikiwa mtakuwa wakaidi
na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua
ninazozichukua hivi sasa" na "Na
ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya
wengine….sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito.
Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".
Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu
raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha"
Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na Pemba…
Nafikiria kuelekea kijiji cha
Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri.
Baada ya dakika 40 nitawamaliza
nyote hasa Wangazija", "
na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa
nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo.
Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa
Waafrika. Mungu Mbariki yeye
na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"
Wakati
unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za
Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa
la chama kimoja lilitangazwa. Lakini
bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani
waliokimbia nchi.
Wanamapinduzi
hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano
wa Tanganyika. Hii ingeruhusu
maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa
baadae katika visiwa hivi.
Askari
polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni
watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo
zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.
Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa
vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar
milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi
wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na mwengine unatarajiwa kufanyika mwaka,
2000.
Viongozi wa kweli na wenye kujali hali za watu wameibuka Tanzania na hii
imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani.
Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya
wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji
mkongwe.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!! MUNGU IBARIKI ZANZIBAR YETU!!
|
0 MAOINI :