LADY JAY DEE APANDA MLIMA KILIMANJARO....
Posted in
No comments
Tuesday, January 8, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Fadhili Athumani, Moshi
MSANII mkongwe katika Tasnia ya muziki hapa nchini, Judith Wambura
maarufu Lady Jay Dee, jana alianza safari ya siku sita ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Lady Jay Dee akiwa ameongozana na Meneja wake ambaye pia
ndiye Mume wake, Gardner Habash, anatarajia kutumia siku sita kupanda mlima huo
mrefu zaidi barani afrika.
Akizungumza na TAIFA LETU.com, katika kilele cha uhuru
kilichoko zaidi ya mita 5859, alisema kuwa lengo la kupanda Mlima Kilimanjaro,
ukiacha programu yake ya kuandaa kipindi chake kinachorushwa na EATV kila siku ya jumapili kiitwacho Diary ya Lady Jay
Dee, anatarajia kutumia nafasi kuhamasisha Watanzania kuupigia kura Mlima huo
kuingia katika Maajabu Saba ya Dunia.
“Lengo langu ukiacha lile la kupiga picha za Diary yangu
inayorushwa EATV, nataka kutumia uwezo wangu na ushawishi wangu kama msanii kuhamasisha
kupanda mlima Kilimanjaro na inatakiwa kila Mtanzania kuthamini, kulinda na
kujivunia urithi huu,” alisema Jay Dee.
Jay Dee alisemakuwa, Watanzania wanatakiwa kujiwekea
utaratibu wa kuupanda na Kuuenzi Mlima Kilimanjaro kila mara na kuongeza kuwa Mlima Kilimanjaro, ambao ni
Mlima mrefu zaidi barani Afrika ni mali na urithi wa kila mtanzania Hivyo ni
vizuri kila mtanzania kujivunia rasilmali tulizonazo kwa kuzitembelea na sio
kuwaachia wazungu pekee.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wasanii kutumia nafasi
waliyonayo kupanda Mlima, kuhamasisha upandaji wa Mlima, na sio kuacha shughuli
hiyo kwa Wageni kutoka nje kuja kututangazia Mlima wetu na kuongeza kuwa ni
vyema kila Msanii kujikita mambo yenye tija na Taifa.
Kwa upande wake, Gasto Mosha ambaye ndiye anayemuongoza
Msanii huyo katika safari yake ya upandaji Mlima, alisema atahakikisha Msanii
huyo anafika kileleni ili aweze kuutangaza vyema Mlima kwa Wasanii kumuunga mkono Lady Jay Dee.
Tanzania’s top celebrity Judith Wambura ‘Lady JayDee’ today
will follow a chain of world’s top celebrity by climbing Mount Kilimanjaro Africa’s
highest point and the world’s free standing mountain through Marangu Route.
As it is known for years Mount Kilimanjaro is one of the world's most famous mountain of which many celebities have conquered including Roman Abrahimovich, Jessica Biel, Justin Timberlake, Lupe Fiasco, Jimy Carter, JBL, and many more
A six days trek was organized
by a local Mount Kilimanjaro experts ‘Kilidove Tours and Safaris Ltd’ of Arusha
Tanzania, during her trek she will be assisted and guided by a team of long
time experienced and reputable mountain tour guides Gastor Mosha and Deogratias
Sosta who also climbed Mount Everest earlier last year for his career.
Along she was joined by her cameraman Justin Bayo, her
husband and a famous Radio presenter Gardner G Habash
Prior to departure she said one of her biggest and longest dream was to
climb and reach top of Kilimanjaro which is Africa’s highest point at
5895metres
all the best ‘Lady JayDee’
all the best ‘Lady JayDee’
Lady JayDee(katikati) Deogratias (kulia) and Gasto Mosha (kushoto) atakayemuongoza Msanii huyo hadi kilele cha Uhuru -Peak 5895m
Lady Jaydee akiwa na mpiga picha wake Justin Bayo katika Geti la Marangu
Lady Jaydee na Gardner Habash baada ya kusaini daftari la Wageni katika Geti la Marangu leo
Lady Jaydee katika pozi kabla ya kuanza kupanda Mlima
Lady Jaydee akitia sahihi katika Daftari la Wageni
kundi la wapandaji kabla ya kupanda Mlima
Mhifadhi Mkuu wa Mlima Kilimanjaro, Erastus Lufungilo akisalimiana na Lady Jaydee kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro zoezi litakalochukua siku sita.Picha ya Pamoja na wapandaji wengin,(kutoka kushoto) Deogratias (guide), Justin Bayo(mpiga picha) Gardner G Habash Mume Wake), Gastor Mosha(guide) Lady Jay Dee, George(Kilidove Tours) Emanuel(porter) and Mr Erastus Lufungilo (Mhifadhi Mkuu)
Lady Jaydee katika Ofisi ya Mhifadhi Mkuu kabla ya Kupanda Mlima Kilimanjaro.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :