WAKAZI WA NJORO YA DOBI, MOSHI WAANZA MWAKA KWA MAJONZI
Posted in
No comments
Wednesday, January 2, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
WAKAZI wa Mtaa wa Dobi, Kata ya Njoro, Wilaya ya Moshi
mjini, Mkoani Kilimanjaro, walijikuta wakianza Mwaka kwa majonzi baada ya
kijana Abdalla Mussa (22), kukutwa akiwa amekufa, Nyumbani katika tukio linalodhaniwa
kuwa ni ya kujinyonga.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana majira ya saa saba
mchana ambapo MTANZANIA iliweza kufika katika eneo la tukio na kukuta maiti ya
Marehemu ikiwa bado imening’inizwa kwa kipande cha kitenge kwenye Nyumba Bovu
lililo karibu na Nyumba ya Mzazi wa Marehemu.
Marehemu kwa mujibu wa Mama Mzazi, Hawa Athumani, alikuwa
anasumbulia na Malaria ambapo wiki mbili kabla ya tukio hilo, Marehemu alikuwa
amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.
“Mwanangu alikuwa anaumwa Malaria na Baada ya kumpeleka pale
Mawenzi madaktari walisema kuwa Malaria imepanda kichwani, alitibiwa na ijumaa
iliyopita tuliruhusiwa kurudi Nyumbani lakini jana (juzi) alianza kulalamika
kuwa kichwa kinauma,” alisema Hawa.
Alisema kuwa siku ya tukio, Marehemu aliamka akiwa mzima
kabisa na hadi tukio la kujinyonga linatokea alikuwa mzima kabisa na wala
hakuonesha dalili zozote za kutia wasiwasi na kuongeza kuwa baadae muda wa saa
Saba mchana, akiwa ameenda sokoni kufanya maandalizi ya sikuukuu, mwanae wa
kiume, alimpigia simu na kumjulisha kuhusu tukio hilo.
Kwa upande mdogo wa Marehemu ambaye alizungumza na Gazeti
kwa masharti ya jina lake kutotajwa Gazetini alisema kuwa Kaka yake muda mfupi
kabla ya kufariki dunia, alikuwa anafanya fujo kwa majirani na kutamka wazi
kuwa lazima, siku patokee msiba lakini kutokana na kufahamu hali yake maneno
yake hawakuyachukulia kwa uzito mkubwa.
“Kaka alikuwa tayari kashajua kufa kwake, alianza kufanya
fujo na kupiga watu ovyo na kusema kuwa siku ya leo lazima mtu afe, sasa sisi
kutokana na kufahamu hali yake wala hatukuchukulia maneno yake siriazi tukaona
labda ni maneno tu.
“ Baadaye kama mwendo wa saa sita na nusu mchana nilishangaa
kuona utulivu usio wa kawaida na nilipoingia chumbani kwake sikumkuta, tukaanza
kumtafuta, kidogo mtoto wa nyumba ya jirani akaja na kuniambia ameona kitu
kimengini akwenye ile nyumba bovu pale, tulienda kuangalia ni nini na kukuta
kaka amekufa,” alisema Mdogo huyo wa Marehemu.
Akizungumza tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa huo, Lucy Peter
Asenga, alisema kuwa, mara baada ya kupata taarifa za msiba huo, aliwasiliana
na Jeshi la Polisi kuomba msaada lakini cha kushangaza pamoja na kutoa Taarifa
mapema, msaada walikuja kuupata masaa mawili baada ya kutoa Taarifa.
Akionesha masikitiko yake katika utendaji na ushirikiano wa
Jeshi hilo mwemnyekiti huyo alisema kama utaratibu wa kutoa msaada wa Jeshi la
polisi hautabadilishwa itafikia muda ambapo wananchi watatafuta msaada kwengine
au kujichukulia hatua wenyewe jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Nchi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio Hilo, Kamanda wa Polisi wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema mwili wa Marehemu
tayari umaeshahidhiwa katika chumba cha Kuhifadhia Maiti ya Mawenzi na kuongeza
kuwa Uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho kinaendelea.
Kamanda Boaz alitumia Nafasi kuwataka wananchi kuepuka
vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha huku akito pole kwa Famila ya Marehemu
kwa Msiba huo uliowakuta.
MWISHO.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :