RADI YAUA MMOJA MLIMA KILIMANJARO
Posted in
No comments
Thursday, January 3, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
HIFADHI
ZA TAIFA TANZANIA
PRESS RELEASE
AJALI
YA RADI YAUA MTALII MMOJA MLIMA KILIMANJARO
Mgeni mmoja raia wa Ireland
anayefahamika kama Ian Mc Keever amefariki dunia jana tarehe 2.1.2013 majira ya
saa sita na nusu mchana baada ya kutokea
kwa ajali ya radi kali wakati akipanda Mlima Kilimanjaro akiwa pamoja na
wenzake.
Ajali hiyo ya radi ilitokea katika eneo
la Kibao cha Moir Hut katika njia ya Londorosi. Aidha, wageni wengine wanne
walijeruhiwa katika ajali hiyo.
Marehemu Mc Keever mwenye umri wa miaka
42 alifika nchini kwa ajili ya shughuli ya utalii ya kupanda Mlima Kilimanjaro
kupitia Kampuni ya Wakala wa Utalii ya Everlasting Tour Company Limited ya
Mjini Arusha ambapo marehemu pamoja na wenzake walianza safari yao ya kupanda
mlima tarehe 30.12.2012
Baada ya kutokea kwa ajali hiyo wageni
wengine 21 waliokuwa pamoja waliamua kuahirisha safari yao ya kupanda mlima.
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa
kushirikiana na Kampuni ya Wakala wa Utalii ya Everlasting zinaendelea na
taratibu mbalimbali za kushughulikia ajali hii pamoja na matibabu kwa
waliojeruhiwa.
Imetolewa na
Pascal Shelutete
Meneja Uhusiano
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
03.01.2013
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :