"POLENI SANA" RAIS KIKWETE AZIFARIJI FAMILIA ZA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA GARI UBENA ZOMOZI
Posted in
No comments
Sunday, February 17, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Magari yaliyosababisha vifo hivyo vya watu tisa wakiwapo wanafunzi wa sekondari ya Chalinze mkoani Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji ndugu,
jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali
ya barabarani maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani
Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa
limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Alifika kuhani ndugu, jamaa na
marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali ya
barabarani maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani
iliyotokea Februari 11, 2013 na kupoteza hapohapo maisha ya watu tisa
wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya
Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli
la mizigo
Familia alizokwenda kuhani na kuzifariji ni pamoja na za marehemu Hassan Erasto Kurunge (57), Maria Sadiki ((52) na mtoto wa mwaka mmoja Samweli Ismail wa kata ya Ubena.
Wengie ni marehemu Essau Enos
Mwamgingo (16) , Stella Isaack Kazimoto (18), Bahati George Mbena (17) na
Latifa Maneno (17)
Akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa
wa Pwani Mhe Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Ahmed Kipozi,
Rais Kikwete alieleza kusikitishwa kwake kwa ajali hiyo, na kuwataka madereva
wawe makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani
Rais Kikwete alisikitishwa zaidi
kwa taarifa kwamba gari hilo dogo lilikuwa limebeba abiria wanane, na kuwa
dereva wake ambaye pia alipoteza maisha, hakuwa makini katika kuzingatia
sheria za usalama barabarani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji ndugu,
jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali
ya barabarani maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani
Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa
limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :