Masanja Mkandamizaji apania Tamasha la Tumaini Jipya
Posted in
No comments
Thursday, March 28, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Masanja alisema kuwa
amejiandaa vyema kutangaza neon la Mungu kwa kupitia kipaji chake cha uimbaji
wa muziki wa Injili, akiamini kuwa afya yake itakuwa njema na kuimba pamoja na
wadau wao katika onyesho hilo la Tumaini Jipya.
Alisema ingawa anatamba sana katika ulingo wa uchekeshaji kwa
kuwa na aina ya uzungumzaji na kufurahisha watu wengi, lakini makali yake
hayaelezeki katika uimbaji wa muziki wa injili.

“Itakuwa ni siku nzuri kwa siku ya Jumapili ya Machi 31
katika uwanja huo wa Jamhuri, hivyo naamini watu watakuja kwa wingi
kulishuhudia neno likipenya masikioni mwao,” alisema Masanja Mkandamizaji.
Mbali na Masanja, wengine watakaofanya onyesho hilo ni pamoja
na Martha Mwaipaja, Stara Thomas, Bahati Bukuku, Sifa John, Joseph Nyuki pamoja
na vikundi mbalimbali vya kwaya vikitajwa kuwapo kwenye tamasha hilo la Tumaini
Jipya litakaloanzia mkoani Morogoro.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :