NANDIPA NA WANAWAKE WENZAKE HATIMAYE WAFIKA KILELENI ; WAFIKISHA UJUMBE WA UKATILI DHIDI YA MWANAMKE KATIKA KILELE CHA UHURU, MLIMA KILIMANJARO
Posted in
No comments
Wednesday, March 6, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Wanawake
10 kutoka nchi za barani Afrika na Asia wameshuka kutoka katika
kilele cha Mlima Kilimanjaro leo baada ya siku 7 za kuzuru Mlima huo maarufu
hapa Ulimwenguni.
WANAWAKE 10 JASIRI BAADA YA KUWASILI GETI LA MWEKA
Miongoni mwa wanawake hao ni
Anna Philipo Indaya Mwanamke wa Kwanza Mhadzabe kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Wengine ni Hlubi Mboya "Nandipa" ambaye ni msanii wa Tamthilia ya ISIDINGO na Balozi
wa WFP Afrika kutoka Afrika Kusini.
Pia Nimdoma Sherpa mwanadada wa
KiNepali na mwenye umri mdogo kuukwea mlima Everest na balozi wa WFP katika kuhamasisha wanawake
kujitambua na kupenda elimu.
wanawake hao 7 kutoka Nepal, Shailee Basnet, vilevile Maya Gurung, Pujan Acharya, Pem
Diki Sherpa, Asha Kumari Singh, Chunu Shrestha.
kutoka Tanzania ni Anna Philipo na Ashura Kayupayupa.Wanawake hao walipokelewa na
viongozi wa WFP na Child Reach International kisha kufanya mahojiano na vyombo
vya habari.
Safari hiyo ya siku sita kupanda mlima Kilimanjaro ni sehemu ya ujumbe wa siku ya Mwanamke duniani na uwezo wa mtu mwanamke ambyo kilele cheke ni Machi 8.
Wanawake hao 10 walidhaminiwa na Shirika la Chakula Duniani, WFP, Childreach International Tanzania na Kinapa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :