DICKSON MARWA ASHINDA NGORONGORO MARATHON
Posted in
No comments
Sunday, April 7, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Fadhili Athumani, Karatu
MWANARIADHA Dickson Marwa kutoka katika timu ya Holili, Kilimanjaro ameibuka mshindi wa mbio za ngorongoro Marathon zilizofanyika Jana wilayani Karatu, Mkoani Arusha kwa kutumia muda wa saa 1:04:49.
Marwa alitumia muda huo katika mbio hizo zinazodhaminiwa na Kampuni ya Tigo kwa mika 6 mfululizo sasa, zilizoanzia katika geti la Ngorongoro umbali wa kilometa 21 na kumalizikia katika uwanja wa Mazingira mjini Karatu.
Katika nafasi ya pili alikuwepo mwanariadha, Stephano Huche kutoka Arusha ambaye alitumia muda wa saa 1:04:56 akifuatiwa kwa karibu na Alphonce Felix wa timu ya Winning spirit ya Arusha aliyetimua mbio hizo kwa muda wa saa 1:05:24.
Washindi wengine katika mbio za kilomeata 21 wanaume ni Calisti Muhindi wa babati akitumia muda saa 1:05:41, Msenduki Muhamedi wa Hanang akitumia muda wa saa 1:05:48, Andrew Sambu wa Hanang pia akifuatia katika nafasi ya sita kwa kutumia muda wa saa 1:05:52 na Damian Chopa wa JKT aliyetumia muda wa saa 1:05:54 akishika nafasi ya saba.
Katika mbio za wanawake mwanariadha Jackline Sakilu wa JWTZ alionesha umwamba wake baada ya kuibuka mshindi akitumia muda wa saa 1:16:26 na kuwaacha Zakia Mrisho wa Team 100 (1:17:47) na Mary Naali wa AAAC (1:18:47) wakimaliza katika nafasi ya pili na tatu mfatano huo.
Awali akizindua mbio hizo Naibu waziri Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliwataka watanzania kuwa wabunifu na kuanzisha mashindano kama haya ili kusiadia kuhamasisha utalii wa ndani na wa nje.
Kwa upande wake Balozi wa Malaria msanii Barnaba Elias alisema kuwa lengo la kushiriki mbio za mwaka huu ni kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu vita dhidi ya Malaria na kuongeza kuwa kwa kutumia michezo na sanaa kampeni hiyo imefanikiwa pakubwa mpaka sasa.
Mshindi wa kwanza katika mbio za mwaka huu kwa upande wa wanaume amejishiundia fedha taslimu shilingi milioni moja, simu ya mkononi kutoka Tigo na medali huku mshindi wa kilometa 21 wanawake akiondoka na fedha taslimu shilingi laki tano, Simu ya mkononi na medali huku washindi wengeni nao wakiondoka na zawadi mbambali.
Mbio za Ngorongoro Marathon zimeandaliwa na kampuni ya kitalii ya Zara Tours kupitia mfuko wake wa Zara charity, Hifadhi ya Ngorongoro, na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo pamoja na washirika wengine.
Mwisho.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :