MATUKIO MUHIMU KATIKA PICHA CHELSEA ILIVYOTWAA UBINGWA EUROPA KATIKA UWANJA WA AMSTERDAM ARENA- UHOLANZI JANA.
Posted in
No comments
Thursday, May 16, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Chelsea wakicheza bila ya John Terry na Hazard chini ya kocha wa muda, Mhispania Rafa Benitez kwenye fainali na Benfica ya Ureno, katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Uropa, Usiku wa Jana waliwaduwaza Wareno, Benfica FC, kwa kuwatandika 2-1 na kutwaa ubingwa huo shukranim ziendee kwa bao la lala salama lililotiwa kimiani na Ivanovic katika dakika ya 94 za mchezo.
Chelsea ndiyo walioanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wao Fernando Torres dakika ya 59 na Benfica nao wakaongeza nguvu na hatimaye mchezaji wa Chelsea kuruka juu na kuunawa mpira eneo hatari la penati na Refa wa Mchezo huo
Bjorn Kuipers kutoka Holland kudai mpira utengwe penati na kisha mchezaji hatari
Óscar Cardozo kuachia mkwaju huo dakika ya 68 na mpira kuishilia nyavuni na kubadilisha matokeo na kufanya 1-1. Dakika za Lala salama Benfica bila wasiwasi na kona hiyo dakika ya nyongeza ya 90 mchezaji Branislav Ivanovic amejitwisha ndoo na kufunga bao na huku kipa wa Benfica Artur Moraes akiangalia mpira huo ukiishilia nyavuni.
Kocha wa England Roy Hodgson naye alikuwepo Amsterdam Arena kushuhudia mtanange huo
Kocha wa Chelsea Rafael Benitez kulia akisuguana na refa kuhusu jambo ambalo limetokea punde uwanjani
Huku Chelsea wakishangilia ushindi huo, Benfica ni taabu kweli kweli.....hoi....
Kwenye patashika..
Hapa kazi tu...
Branislav Ivanovic ameifungia bao kwenye muda wa lala salama
Mchezaji Frank Lampard akiangalia mambo juu ya mambo uwanjani Amsterdam Arena kabla ya kufungana kipindi cha pili.
Mchezaji wa Benfica Luisao akizuia shuti la Ramires
Oscar Cardozo akijiuguza baada ya kuisawazishia Benfica na kwa mkwaju wa penati na kufanya 1-1
Cesar Azpilicueta hoi baada ya Oscar Cardozo kufunga bao kwa mkwaju wa penati
Fernando Torres ndiye aliyeanza kuifungia bao Chelsea kwa kumchenga hadi kipa wao Benfica
VIKOSI:
Benfica: Artur Moraes, Almeida, Luisao, Garay (Jardel 78), Melgarejo (John 66), Perez, Matic, Rodrigo (Lima 66), Gaitan, Cardozo, Salvio.
Subs: Paulo Lopes, Aimar, Urreta, Gomes.
Goal: Cardozo 68pen.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Lampard, Luiz, Ramires, Mata, Oscar, Torres.
Subs: Turnbull, Mikel, Moses, Ferreira, Marin, Benayoun, Ake.
Goal: Torres 60, Ivanovic 90+3.
Referee: Bjorn Kuipers
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :