DULLY SYKES KUPAMBA USIKU WA REDDS MISS MOSHI 2013 AVENTURE

Posted in
No comments
Thursday, May 16, 2013 By danielmjema.blogspot.com



Dully Sykes
 Na Mwandishi Wetu, Moshi

MSANII wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Dully Sykes "mista Misifa" anatarajia kupanda jukwaani kutumbuiza katika usiku wa Ulimbwende, usiku wa Redds Miss Moshi 2013 yatakayofanyika May 18, katika ukumbi wa Aventure, Mjini Moshi.

Akizungumza na Taifa Letu.com, mratibu wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa kampuni ya New Vision plan inayohusika na kazi za kuandaa  mashindano ya ulimbwende, Moses Komba alisema kuwa jumla ya warembo19 watachuana kumsaka malkia wa Moshi wakisindikizwa na Prince Dully Sykes.

Moses alisema tayari maandalizi yameshaanza na mchujo wa kwanza umeshafanyika ambapo warembo  wote wameshaingia kambini kujifua na kuongeza kwamba mashindano ya mwaka ambayo ni ya pili tangu yaanzishwe yatakuwa ni ya aina yake.

“Maandalizi yameshaanza, warembo wote wapo kambini hapa katika ukumbi wa Aventure, kutoa burudani atakuwepo mtu mzima Prince Dully Sykes, kila kitu kinakwenda sawa na tunategemea kushuhudia kitu tofauti na yale ya mwaka jana,” alisema Komba.

Kuhusu swala la udhamini alisema bado hilo ni tatizo huku wadhamini wakuu Redds na kampuni ya panone kwa kujitolea kudhamini mashindano hayo. Akitangaza viingilio katika mashindano ya mwaka huu, Komba alisema kuwa kwa viti vya dhahabu viingilio vitakuwa sh. 50,000, viti vya V.I.P vitakuwa ni sh. 30,000 na viingilio vya kawaida ni sh. 15,000.

Kwa upande baadhi ya washiriki wa Redds Miss Moshi, wakizungumza na Gazeti hili katika kambi ya mazoezi, Jacky Mushi, Winlady Mushi, Aichi Edwin na Rayness White walisema kuwa wabnatarajia kutumia uzoefu watakaoupata kutoka katika mashindano hayo kulitumikia jamii hasa wale waishio katika mazingira magumu.

Mashindano ya Redds Miss Moshi 2013 yatakayofanyika katika ukumbi wa Aventure, yanadhaminiwa na Redds, Panone na Baba G na Zoom Net Printers ambapo kwa upande wa burudani alisema atakuwepo msanii mkongwe wa kizazi kipya Dully Sykes akisindikizwa na wasanii wengine kutoka Moshi.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .