M23 WADAIWA KUBAKA NA KUUA DRC
Posted in
No comments
Tuesday, July 23, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Haya yalikuwa mashambulizi ya kwanza tangu vita kati ya pande hizo mbili kuanza Jumatatu asubuhi na kusitishwa siku hiyo mchana.Kundi hilo limesema liko umbali wa kilomita nne kutoka mji wa Goma, ingawa limesema lengo lake ni kulazimisha serikali kufanya mazungumzo nao wala sio kuteka mji wa Goma.
M23 liliuteka mji wa Goma, kwa siku kumi mwezi Novemba kabla ya kuondoka mjini humo kufuatia shinikizo za jamii ya kimataifa kufanya mazungumzo na serikali ya rais Joseph Kabila.Mazungumzo na serikali yalianza mjini Kampala mwezi Disemba ingawa baada ya miezi miwili jeshi likaanza tena mapigano na waasi hao mwezi Julai tarehe 14.Kulingana na Umoja wa Mataifa mapigano hayo yamesababisha takriban watu 4,200 kutoroka makwao.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :