RAIS KIKWETE AMTEUA BALOZI LUMBANGA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA PPRA

Posted in
No comments
Tuesday, July 23, 2013 By danielmjema.blogspot.com

NA JENNIFER CHAMILA- MAELEZO
 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amemteua Balozi Matern Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Manunuzi Serikalini ( PPRA).
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari  na  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya PPRA   Laurent Shirima imeeleza kwamba uteuzi huo , umeanza  rasmi kuanzia  Juni 20 ,mwaka huu ambapo Balozi Lumbanga amechukua  nafasi ya Dk. 
 
 Enos Bukuku aliyemaliza muda wake katika uongozi huo.Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Balozi Lumbanga ni mchumi kitaaluma,ana Shahada ya kwanza ya Uchumi ambayo ameipata katika Chuo Kikuu cha Dares salaam(UDSM).
 
Pia ana Shahada ya Uzamili pamoja na Shahada ya Uzamivu katika masuala ya Mahusiano ya Kimataifa taaluma aliyoipata  chuo cha Geneva School of Dipmacy and International Relations, Switzerland.
 
Balozi Lumbanga ameitumikia Serikali ya Tanzania katika nyazifa mbalimbali tangu mwaka 1972,mwaka 1995 aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi nafasi alioishika hadi mwaka 2006 alipoteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) nchini Geneva.
 
Amestaafu utumishi wa umma  Julai mwaka jana (2012).
 
Balozi Lumbanga amekuwa Mwenyekiti wa tatu wa bodi  ya PPRA tangu ilipoanzishwa mwaka 2005 ambapo Mwenyekiti wa kwanza alikuwa Bw.Philemon Luhajo na kufuatiwa na Dk.Bukuku. 
 
KWA MSAADA WA: Father Kidevu

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .