RAIS KIKWETE AKABIDHI NYUMBA 8 KWA WAHANGA WA MAPOROMOKO SAME
Posted in
No comments
Thursday, July 11, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, ametekeleza ahadi yake aliyoitoa kwa wakazi wa
kijiji cha Goha, kata ya Mamba Myamba, Tarafa ya Myamba, wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kwa kukabidhi Nyumba nane wahanga wa
Maporomoko yaliyotokea mwishoni mwa mwaka 2009.
Mkurugenzi wa wilaya ya Same, Joseph Mkude, akitoa taarifa ya ujenzi wa Nyumba hizo 8 |
Gama akisalimiana na mmoja wa wahanga wa maporomoko ya Same, Eliamini Charles (5), ambaye alipoteza wazazi wake wote katika Maporomoko hayo kabla ya kumkabidhi Nyumba moja kati ya Nyumba 8 za JK. |
Gama akizindua nyumba 8 za JK Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi akimpongeza |
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, katikati ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Same, Christopher Irira, na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Wilaya Same, Joseph Mkude |
RC-Gama akizungumza na wahanga wa Maporomoko ya Same kabla ya kukabidhi Nyumba 8 ambazo ni sehemu ya ahadi za JK kwa wahanga wa Maporomoko hayo yaliyotokeas mwaka 2009. |
Gama akifungua Nyumba kama sehemu ya utekelezaji wa Ahadi ya JK kwa wahanga wa maporomoko, kushoto kwake ni mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi. |
Gama akiwa na mkandarasi wa majengo hayo |
Mkurugenzi wa Wilaya ya Same Joseph Mkude akitoa maelezo kwa Gama wakati wa makabidhiano ya Nyumba za JK |
Ahadi hiyo ya Rais Kikwete aliitoa alipotembelea maeneo yaliyothiriwa na Maporomoko ya Ardhi yalitokea kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo hayo na Tanzania nzima na kusababisha vifo vya watu 24 huku wengine 45 wakikosa makazi.
Akikabidhi nyumba hizo jana kwa
niaba ya Rais, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama amesema kuwa hiyo ni
ahadi ya Rais Kikwete, aliyoitoa wakati alipo watembelea wahanga hao, mwishoni
Mwa Novemba 2009 na kuahidi kuwajengea nyumba nane wahanga hao wakati alipowatembelea
na kuwafariji.
Katika taarifa yake hiyo iliyosomwa
na Gama, Rais Kikwete amesema serikali yake inafanya juhudi zote kuhakikisha
kuwa wananchi wake wanapata maisha bora ikiwa ni pamoja na makazi bora kwa kila
mtu lengo ambalo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM na moja ya ahadi zake
kipindi cha uchguzi.
Aidha amewataka wakazi wa maeneo hayo kuepuka watu wanaojipitisha wakiwalaghai kwa maneno ya kuwalaghai kuwanunulia nyumba hizo na kutoa agizo kwa uongozi wa wilaya kuzisimamia nyumba hizo ili wasiwepo watu wa kubadili umiliki wa nyumba za wahanga hao kwenda kwa umiliki wa watu wengine.
Awali akitoa taarifa fupi amesema katika fedha hizo, ofisi ya waziri Mkuu kitengo cha maafa kilituma shilingi milioni 162, 376,000, huku benki ya NMB ilitoa mchango wa wa saruji mifuko 100 na mabati 400 vyenye thamani ya shilingi milioni 9,757,650.

Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :