KAVISHE: "TAIFA STARS BADO INA NAFASI YA KUWAPA RAHA WATANZANIA"
Posted in
No comments
Thursday, July 11, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa
mchezaji wa Timu ya Taifa, Shomari Kapombe, Jijini Dar es Salaam wakati
wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao
ni wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa
wachezaji wote na benchi la ufundi.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa
Nahodha wa Timu ya Taifa, Juma Kaseja Jijini Dar es Salaam wakati wa
chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni
wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa wachezaji
wote na benchi la ufundi.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa
mchezaji wa Timu ya Taifa, Salum Abubakar, Jijini Dar es Salaam wakati
wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao
ni wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa
wachezaji wote na benchi la ufundi.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa
mchezaji wa Timu ya Taifa, John Bocco, Jijini Dar es Salaam wakati wa
chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni
wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa wachezaji
wote na benchi la ufundi.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa
mchezaji wa Timu ya Taifa, Nardil Haroub (Cannavaro), Jijini Dar es
Salaam wakati wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro
Premium Lager ambao ni wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo
zilikabidhiwa kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa Kocha
wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen, Jijini Dar es Salaam wakati wa chakula
cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni
wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa wachezaji
wote na benchi la ufundi.
**************
Wadhamini
wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kilimanjaro Premium Lager, wamewataka
watanzania kutokata tamaa licha ya Taifa Stars kutofuvu kucheza Fainali
za Kombe la Dunia Brazil mwakani kwani timu imeonesha uwezo wa hali ya
juu mpaka sasa.
Ombi
hilo lilitolewa na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George
Kavishe wakati alipowaandalia Taifa Stars chakula cha jioni katika
hoteli ya Tansoma ikiwa ni utaratibu wa wadhamini hao kama njia ya
kuwakaribisha wachezaji kambini.
Alisema bado kuna mashindano mengine kama CHAN na AFCON ambayo wana imani Taifa Stars itafuzu na kwuweka historia.
Aliwaasa
wachezaji kuhakikisha wanashinda mechi dhidi ya Uganda haa nyumbani na
pia watakapoenda Uganda baadaye mwezi huu katika mechi ya kuwania kufuzu
mashindano ya CHAN mwakani nchini Afrika Kusini.
“Tumeshindwa kufuzu kwenda Brazil basi twende Afrika Kusini mwakani,” alisema Bw. Kavishe.
Alisema wao kama wadhamini wamefarajika kuona jinsi Timu ya Taifa imepiga hatua tangu waanze kuidhamini mwaka jana.
“Vilabu
vya Simba na Yanga zilikuwa na nguvu sana na moja ya dhamira zetu kama
wadhamini ilikuwa ni kuinua kiwango cha Taifa Stars na kufanya
watanzania warudishe imani kwa timu yao na sote ni mashuhuda kwani
katika mechi ya kwanza kabisa mwaka jana uwanja ulikuwa na watu 10,000
tu lakini katika mechi dhidi ya Ivory Coast hivi majuzi uwanja ulijaa
kabisa,” alisema.
Meneja
huyo pia alitumia nafasi hiyo kutoa zawadi maalumu kwa wachezaji hao
ambazo ni pamoja na DVD zilizorekodiwa maelezo (profiles) za kila
mchezaji, kazi ambayo ilifanywa kitaalamu kwa udhamini wa Kilimanjaro
Premium Lager.
Wachezaji wataweza kutumia kazi hizi kwenye mitandao ili waweze kujulikana vizuri ndani na nje ya nchi.
“Tulisema
tunaijenga timu na timu inajengwa na wachezaji na ndio maana tumeamua
kufanya kazi kama hizi ambazo zitapandisha hadhi ya wachezaji,” alisema
huku akitoa wito kwa vilabu kutosita kuaruhusu wachezaji wakati wanaitwa
kurekodi kazi kama hizo.
Kwa
upande wake, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen aliwashukuru
wadhamini na kusema, “Kwa kweli mumekuwa zaidi ya wadhamini maana
ushirikiano mliioonesha ni wa hali ya juu.”
Alisema wachezaji wana ari kubwa sana kwani matunzo wanayopata sasa hivi ni ya hali ya juu na wote wanalenga kupata mafanikio.
Taifa
Stars iko kambini kuanzia Julai 4 mwaka huu ikijiandaa na mechi dhidi
ya Uganda Jumamosi hii na mechi ya marudiano itapigwa wiki mbili zijazo
Mjini Kampala ili kuwania kufuzu katika mashindano ya CHAN.
KWA HISANI: Fadher Kidevu
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :