GERARDO MARTINO KUMRITHI VILANOVA BARCA

Posted in
No comments
Tuesday, July 23, 2013 By danielmjema.blogspot.com


GERARDO_MARTINORAIA wa Argentina, Gerardo Martino, Kocha wa Newell’s Old Boys ya huko Argentina, anatarajiwa kutangazwa kuwa Meneja mpya wa FC Barcelona kuchukua nafasi ya Tito Vilanova alieondoka kwa sababu za kiafya.
Martino, mwenye Miaka 50, anategemewa kusaini Mkataba wa Miaka mitatu na kutangazwa rasmi baadae Wiki hii.

WASIFU WAKE:

JINA: Gerardo Daniel Martino
KUZALIWA: Novemba 20, 1962 (Miaka 50), Rosario, Argentina
TIMU ya VIJANA: Newell's Old Boys
KLABU:
1980–1990  Newell's Old Boys Mechi 392  Magoli: 35
1991 Tenerife Mechi 15 Goli: 1
1991–1994  Newell's Old Boys Mechi: 81 Goli: 2
1994–1995   Lanús Mechi 30 Goli 3
1995 Newell's Old Boys Mechi 15
1996 Barcelona SC Mechi 5
ARGENTINA: Mechi 1
UMENEJA:
1998 Brown de Arrecifes
1999 Platense
2000 Instituto
2002–2003   Libertad
2003–2004   Cerro Porteño
2005 Colón
2005–2006   Libertad
2006–2011   Paraguay
2012–2013   Newell's Old Boys
2013-           Barcelona FC

Akiwa Nou Camp, Gerardo Martino atakuwa pamoja na Wasaidizi wake mwenyewe ambao ni Elvio Paolorrosso, Kocha wa Viungo, na Msaidizi Jorge Pautasso.Awali ilitegemewa Kiungo wa zamani wa Barca, Luis Enrique, ndie atatwaa madaraka Nou Camp lakini tatizo kubwa ni kuwa Enrique alijiunga na Klabu ya La Liga Celta Vigo Mwezi uliopita tu na ukaja utata wa Mkataba.

Martino, au ‘Tata’ kama alivyo maarufu, anakuwa Muargentina wa nne kuwa Kocha wa Barcelona wengine ni Helenio Herrera, Roque Olsen na Cesar Luis Menotti na anatua Nuo Camp kuungana na Supastaa wa Argentina Lionel Messi ambae amemsifia sana Kocha huyu.

Jumatano, Barcelona inacheza Mechi ya Kirafiki na Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich na itakuwa chini Jordi Roura kwenye Mechi hiyo iatakayochezwa huko Allianz Arena, Munich.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .