MOURINHO KUWAKOSA AZPILICUETA, MATA, TORRES MWANZO WA LIGI!

Posted in
No comments
Tuesday, July 23, 2013 By danielmjema.blogspot.com


MOURINHO-CHELSEA_TRAININGMSIMU mpya wa Ligi Kuu England utaanza Agosti 17 na tayari Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ashapiga hesabu zake na kugundua katika Mechi ya ufunguzi ya Ligi ya Timu yake dhidi ya Hull City upo uwezekano mdogo kwa Wachezaji wake wanaocheza Timu ya Taifa ya Spain kucheza Mechi hiyo iliyopangwa Agosti 18.

Vile vile, Mourinho sasa anatafakari Wachezaji gani awatoe kwa Mkopo kwa ajili ya Msimu mpya.

Tatizo kwa Mourinho ni kuwa kabla Ligi kuanza zipo Mechi za Kimataifa za Kalenda ya FIFA na Chelsea inawajibika kuwaachia Wachezaji wake kwenda huko na miongoni mwao wapo Wachezaji watatu wa Spain, Juan Mata, Fernando Torres na César Azpilicueta, ambao watarudi tena kujiunga na Chelsea yakiwa yamebaki chini ya Masaa 24 tu kabla Chelsea haijacheza na Hull City Uwanja wa Stamford Bridge.

Agosti 14 Spain watacheza huko Mjini Guayaquil Nchini Ecuador na Timu ya Taifa ya Nchi hiyo na Siku hiyo hiyo Uwanjani Wembley, England itacheza na Scotland.

Mourinho amesema: “”Kikosi changu cha Mechi ya Hull kitategemea Wachezaji hao hao watakaocheza Mechi za Kimataifa Siku mbili kabla! Ikiwa Mtu anaenda Ecuador na kurudi London Jumamosi baada ya Masaa 15 angani sidhani ataweza kucheza Jumapili!””
Tatizo hili za Mechi hizi za Kimataifa kuchezwa Siku mbili tu kabla Ligi kuanza limelalamikiwa sana na Mameneja wengi wa Ligi Kuu.Wakati huo huo, Mourinho ametoboa kuwa sasa anatafakari Wachezaji gani Chipukizi awatoe kwa Mkopo kwa ajili ya Msimu ujao.

Jumanne Chelsea wanatua Jakarta, Indonesia ambako Alhamisi watacheza na Indonesia All Stars XI na Mechi hizi ni muhimu kwa Mourinho kuwapima Chipukizi wake.Mmoja ambae atazikosa Mechi hizi ni Kevin De Bruyne ambae aliumia huko Malaysia na kurudishwa London lakini wengine kama Romelu Lukaku wapo Kikosini.

Tayari Mourinho ameshaamua kuwatoa kwa Mkopo Nathaniel Chalobah, Lucas Piazón na Josh McEachran ili wapate uzoefu.Chipukizi ambae ataingizwa Kikosi cha Kwanza ni Sentahafu toka Czech, Tomas Kalas, Miaka 20, ambae alinunuliwa kutoka Sigma Olomouc Mwaka 2010 na kukaa kwa Mkopo huko Vitesse Arnhem kwa Miaka miwili.

Mwingine ni dogo wa Burkina Faso, Bertrand Traore, Miaka 17, ambae Mourinho amethibitisha kuwa atapewa Mkataba wa Mchezaji wa Kulipwa akifikisha Miaka 18.

CHELSEA-ZIARA:

May 24 Manchester City (Busch Stadium, St Louis)=KIPIGO 3-4
May 25 Manchester City (Yankee Stadium, New York)=KIPIGO 3-5
Julai 17 Singha All-Stars (Rajamangala Stadium, Bangkok)=USHINDI 1-0
Julai 21 Malaysia XI (Kuala Lumpur - BNI Cup 2013) =USHINDI 4-1
Julai 25 BNI Indonesia All-Stars (Gelora Bung Karno National Stadium, Jakarta) SAA 10 JIONI
Agosti 2 Inter Milan (Lucas Oil Stadium, Indianapolis - Guinness International Champions Cup) SAA 9 USIKU

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .