MASHINDANO YA NGALAWA YAFANA TANGA
Posted in
Michezo
No comments
Monday, February 3, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Muheza
Mashindano ya ngalawa yaliyofanyika jana Wilayani Muheza katika
Kijiji cha Kigombe yamefana huku Kampuni ya simu ya ZANTEL ikifanikisha kwa kutoa zawadi.
Ngalawa zikiwa katika mstari kwa ajili ya kuanza mashindano katika pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza. |
Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau (CUF),
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo amewataka vijana washiriki
katika michezo badala ya kukaa vijiweni.
Kauli hiyo aliitoa wakati
akifungua mashindano ya kwanza ya Ngalawa mkoani Tanga yaliyofanyika
kwenye Pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.
Mwidau alisema kupitia
michezo vijana wataweza kupata fursa nyingi ikiwemo elimu na ujunzi kutoka kwa
wenzao ,burudani pamoja na kujenga afya za kimwili na kiakili.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa
Tanga Amina Mwidau (CUF), kizindua mashindano ya Ngalawa Wilayani Muheza.
|
“Mahindano haya ya Ngalawa
hapo awali yalikuwa yanafanyika ngazi ya kijiji lakini kupitia kwa wadhamini Kampuni
ya simu ya ZANTEL tumeweza kuyafanya kimkoa kwa lengo la kuibua fursa za ajira
kwa vijana na kwashirikisha watu katika michezo, ”alisema Mwidau.
Nae Meneja mauzo
wa ZANTELTanzania Salum Ngururu, alisema kuwa
lengo la kudhamini mashindano hayo ni kurudisha faida wanayopata kwa
jamii kutoka na huduma zake na kuendelea kuwatambulisha bidhaa zinazotolewa na
kampuni hiyo.
Meneja mauzo wa ZANTELTanzania Salum Ngururu, akikamkabidhi zawadi mshindi wa kwanza katika mashindano ya Ngalawa, Juma Mgeni zawadi yake. |
Alisema ZANTEL itakuwa ikiboresha zawadi za mashindano hayo
kila mwaka ili yaweze kuvuta washiriki wengi.
Mshindi wa kwanza alijipatia kitita cha Shilingi laki tatu,
kikombe cha ushindi pamoja na medali za dhahabu.Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka ambaye
aliweza kujinyakuliwa zawadi hiyo.
Sehemu ya umati wa wananchi wakifuatilia michuano ya Ngalawa. |
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya Ngalawa thelathini
zilizokuwa na washiriki watano ambapo washiriki walitoka katika Wilaya za
Tanga, Pangani na Muheza huku Wilaya ya Mkinga ikishindwa kushiriki kutokana na
kushindwa kufanya maandalizi mazuri.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :