Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 05.05.2018

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 05.05.2018

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anamtolea macho mshambuliaji wa Napoli, Dries Mertens. Mchezaji huyo mwenye miaka 30 amefunga magoli 45 katika kipindi cha misimu miwili iliyopita kwenye ligi ya Serie A.(Sun).
Kiungo mshambuliaji raia wa Algeria, Riyad Mahrez ametupilia mbali ombi la kuondoka Leicester lakini Mahrez mwenye miaka 27 bado hajatulia katika timu yake ya Leicester. (Sky Sports)
Mrithi wa Arsene Wenger atapatiwa bajeti ya usajili kiasi cha pauni milioni 200, huku Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri akipigiwa upatu kushika mikoba ya Wenger.
Hata hivyo, Arsenal na Chelsea wanamtaka Kocha wa Monaco,Leonardo Jardim, ambaye anatarajiwa kuiacha klabu hiyo mwishoni mwa msimu.(Sun)
AC Milan wanataka kumchukua kiungo wa kati wa Manchester United, Marouane Fellaini (30) raia wa Ubelgiji. Mchezaji huyo atamaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi June.(Corriere dello Sport via Talksport)
Kiungo mshambuliaji wa Everton, Kevin Mirallas amevunjiwa mkataba na klabu ya Olympiakos. Amefunga magoli mawili katika michezo 13 ya ligi kuu ya Uturuki. (Liverpool Echo)
Mabingwa wa ligi daraja la kwanza Wolves wanataka kumsajili mlinda mlango wa Southampton,Alex McCarthy (Mirror)
Kiungo wa kati wa Arsenal Santi Cazorla amesema hajapatiwa mkataba mpya, mkataba anaoutumikia sasa utaisha kipindi cha majira ya joto(ESPN)
Kiungo mshambuliaji wa Manchester City Yaya Toure anataka kuendelea kucheza ligi kuu .Toure ataondoka City mwishoni mwa msimu baada ya miaka minane Etihad.(Manchester Evening News)
Kocha wa Palace, Roy Hodgson amesema ''hana mpango'' wa kustaafu.Hodgson, mwenye miaka 70, amebakisha mwaka mmoja kumaliza mkataba wake. (Evening Standard)

Peter Crouch amesema ataangalia mustakabali wake iwapo Stoke itashuka daraja msimu huu. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 37 alisaini mkataba wa mwaka mmoja mwezi Novemba. (Sky Sports)
Mlinzi wa kati Aston Villa John Terry amesema ataendelea kubaki Villa Park kwa msimu mwingine iwapo watapanda ligi kuu. Kapteni huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England alitia saini mkataba wa mwaka mmoja majira ya joto mwaka hana baada ya kuondoka Chelsea. (Manchester Evening News)
Kocha mpya wa Rangers, Steven Gerrard anamnyemelea aliyekuwa mchezaji mwenzake kwenye kikosi cha Liverpool, Martin Skrtel kuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza kusajiliwa . Skrtel anaichezea klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.(Daily Record)
Mlinda mlango wa Watford, Orestis Karnezis anataka kurejea nyumbani, Ugiriki, Mchezaji huyo (30) amesema anapenda kuichezea Olympiakos.(Watford Observer)

Tuliwapa Salah na De Bryune 'Second Chance' iweje tusimpe Balloteli

Tuliwapa Salah na De Bryune 'Second Chance' iweje tusimpe Balloteli

No comments
By danielmjema.blogspot.com
LONDON, ENGLAND


Ni ngumu kufananisha maji na mafuta, hilo halina ubishi, lakini kama Soka la Uingereza liliweza kumuamini Mohammed Salah na kumpa ‘second chance’, akaonesha alichonacho, kwanini ishindwe kumuamini mtukutu Mario Balotelli?

Kwanini ilikuwa rahisi kuamini kuwa Salah amebadilika halafu ishindwe kuamini kuwa Balloteli ameacha utukutu na kwamba sasa yuko tayari kucheza soka?

Mwaka 2011, Chelsea walitangaza kumsajili Mohammed Salah, kwa pauni milioni 11, lakini baada ya kushindwa kuonesha makali yake, akapelekwa Fiorentino na Roma kwa ahadi ya kurudi atakapo kuwa tayari kucheza
soka.

Ni kweli Salah, alipohakikisha ameiva, alirejea England, mwenyeji wake akiwa ni Liverpool. Salah akauhakikishia umma wa wapenda nchini England, kwamba sasa yuko tayari kucheza soka la uhakika. Tulimuamini na kilichotokea ni kama mlivyosikia.

Kama ilivyokuwa kwa Salah, Kevin De Bryune alitua England mwaka 2012, akitokea Ubelgiji. Akasajiliwa na Chelsea, lakini kwa bahati mbaya wakati huo, bado hakuwa tayari kucheza soka, ikabidi aondoke kwa ahadi
ile ile, ya kurejea atakapokuwa tayari.

Na kweli, mwaka 2015, baada ya kuzuruza kila mahali kutafuta uzoefu, De Bryune alirejea na kutua pale Etihad. Akatuaminisha kuwa ni kweli amebadilika na kama kawaida wapenda soka tulimuelewa tukampa ‘second
chance’. De Bryune hajatuangusha kuanzia hapo.

Unaweza kujiuliza ni  kwanini nimewataja wanaume hawa, wakati muhusika ni Super Mario Balloteli. Ni hivi, kati ya mwaka 2010 na 2013, Balloteli alikuwa mchezaji wa Manchester City, hata hivyo hakukaa, akaondoka.

Kilichomuondoa Balloteli pale Etihad (City of Manchester), hakina tofauti sana na kilichowaondoa De Bryune na Salah wakati ule; hakuwa tayari kucheza, tena yeye kesi yake ilikuwa tofauti kwa maana kwamba, alikuwa amezidiwa na ‘utoto’

Mwaka 2013, baada ya kuondoka England alielekea Italia ambako alijiunga na AC Milan. Akaichezea jumla ya michezo 43 na kufunga mabao 26. Mwaka 2014, akiamini yuko vizuri, alirejea England na kutua Liverpool. Hata hivyo, hakuwa na jipya, katika mechi 16, aliishia kufunga bao moja tu.

Liverpool, wakamuambia akajifue akiwa tayari watamfikiria. Wakamrudisha AC Milan kwa mkopo. Aliporejea AC Milan, Balloteli aliwaomba radhi wapenzi wa mchezo wa soka duniani kote na kuwahakikishia kuwa amebadilika na yuko tayari kucheza soka.

Akizungumzia mchezaji huyo, Kocha wa Liverpool wakati huo, Brendan Rogers, alituhakikishai namna ambavyo Balloteli amebadilika na yuko tayari kucheza soka. Alisema Muitaliano huyo sasa amekuwa na kwamba ameacha utoto. Wote walitundanganya!

Akaingia dimbani mara 20 na kufunga bao moja. Mwaka 2016, Liverpool ikampiga bei mazima katika klabu ya Nice, inayoshiriki Ligue 1, nchini Ufaransa. Kuanzia hapo akaanza kuonesha kubadilika, katika mechi 46, amefanikiwa kufunga mabao 29!

Akiwa na miaka 27, Balloteli sasa hivi anaonesha dalili za kupevuka. Baada ya kukaa nje ya soka la ushindani kwa zaidi ya miaka miwili, haimanishi kwamba Ligue 1 hakuna ushindani, lakini kwa kuzingatia mwenendo wa soka la Balloteli, ashakum sio matusi, alikuwa lupango.
 

Muitaliano huyu, hivi sasa anaonesha utayari wa kurejea kwenye ulimwengu wa soka. Msimu huu ameingia dimbani mara 33 na kufumania nyavu mara 22. Huu ni muendelezo wa alichokifanya msimu uliopita ambapo alifunga mabao 15, katika mechi 23.

Yote hayo Balloteli ameyafanya bila ya kujikuta katika matukio ya kitoto kama kupigana klabuni. Ili kuthibitisha kuwa kwa kweli amebadilika, hakuna siku hata moja amejikuta akiingia katika mvutano na kocha wake wala wachezaji wenzake.

Kuna tetesi kuwa, Muitaliano huyo yuko tayari kurejea England. Hapa ndipo hoja yangu inapoanzia, Endapo itathibitika kuwa ni kweli Balloteli anataka kurudi England, Je tutakuwa tayari kumpokea na kumpa ‘second chance’ kama tulivyofanya kwa Salah na De Bryune?

Kuna madai kuwa, Jose Mourinho anafikiria kumrejesha nyota huyo wa zamani wa Manchester City na Liverpool. Kama hilo litatokea itakuwa ni habari nzuri. Lakini swali ni je tunaweza kumuamini Balloteli? Akirudi
ataendeleza moto wake, au atafufua vituko vyake?

Hivi sasa anachokifikiria ni kushiriki michuano mikubwa. Balloteli anawaangalia Mohammed Salah na Kevin De Bryune na kujikuta akitamani kupata mafanikio makubwa katika soka, ikizingatiwa kuwa, umri wake
haumpi uhakika wa kuendelea kuwa na kiwango alichonacho sasa baada ya miaka miwili.

Ukweli huu ndio unaowapa hofu viongozi wa Nice na benchi la ufundi la klabu hii kwa sasa. Wanafahamu kuwa hawana uwezo tena wa kumpa anachokitaka katika umri huu wa miaka 27. Kwa sasa Balloteli anahitaji
mafanikio, anataka kubeba mataji. Rais wa Nice, Jean-Pierre Rivere, analithibitisha hilo:

“Bila mashinano ya Ulaya, itakuwa ngumu kumshawishi kwa sasa, ni wazi kuwa hatuna nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa, Kombe la Uropa nao ni mfupa mgumu kwetu, kwa hali naona akiondoka, ni moto wa kuotea mbali
uwanjani, amebadilika sana, hata staili yake ya uchezaji umebadilika pakubwa.”

Kama kuna kitu cha kujifunza kutoka katika msimu huu wa soka wa ligi kuu ya England, ni kwamba hata nyota wenye majina makubwa, huwa wanahitaji muda na changamoto ya kuwajenga na kuwafanya wawe na ubora
walioa nao.

Mfano hai ni Kevin De Bryune wa Man City na Mohammed Salah wa Liverpool. Hata Cristiano Ronaldo mwenyewe ilibidi aondoke Sporting Lisbon, apitie katika mikono salama ya Sir Alex Ferguson kabla ya kuwa staa wa dunia tunayemshudia pale Santiago Bernabeu.

Kama kigezo cha umri ndicho kitakachosababisha soka la England na mashabiki wake wamkatae Balloteli kwa sasa, basi kuna haja ya kurudi maktaba na kutafuta kitabu cha Jamie Verdy, kulisoma na kuelewa maana
halisi ya mafanikio na Umri.

Kama Verdy aliweza kuipa Ubingwa Leicester katika umri wake mkubwa wa miaka 30, kwanini ishindikane kwa Balloteli na miaka yake 27? Maana yangu ni kwamba hakuna umri maalum, au wakati maalum wa kufanya
kilichosahihi.

Mario Balloteli Barwuah, wa sasa sio yule tuliyemzoea, Balloteli wa sasa ni Baba wa watoto wawili, Lion na Pia. Anarudi kwetu akiwa ni mtu mzima. Anajua ni kipi kinachomstahili kama Baba wa familia. Huu ndio wakati ambao tunaweza kukishuhudia kipaji halisi cha Balloteli. Majukumu aliyonayo yanamsukuma kujituma.

Mwenyewe amekiri kuachana na zile tabia za kupgana Baa. Amekiri kuachana na tabia za kukimbizana na vibinti vidogo katikati mwa Jiji la London na Manchester kama ambavyo alizoea kufanya kipindi. Anasema kabadilika kwanini tushindwe kumuamini kama tuliweza kuwaamini Salah na De Bryune?

Mwisho.

KIUNGO WA ZAMANI WA TAIFA STARS ATHUR MWAMBETA ANAOMBA MSAADA

KIUNGO WA ZAMANI WA TAIFA STARS ATHUR MWAMBETA ANAOMBA MSAADA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Simba Sports iliyokuwa ikiitwa Senderland ,Athur Mwambeta amewaomba wadau mbalimbali wa mchezo wa soka nchini na Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsaidia kupata chombo cha usafiri kitakachomtoa sehemu moja mpaka nyingine mara baada ya kukatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi yanayomkabili.
 


Mwambeta amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na Globu ya jamii katika hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo amelazwa katika jengo la Kibasila ward namba 11, ambapo anaendelea na matibabu mara baada ya kukatwa mguu ijumaa iliyopita.
 


"Nimeugua maradhi haya pindi tu nilipoacha kucheza mpira hali iliyopelekea kukatwa mguu wangu wa kwanza mwaka 2015 na mwaka huu ijumaa iliyopita ndipo nilipokatwa mguu wangu wa pili na kubaki kama hivi mnavyoniona, kwani siwezi tena kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama ilivyokuwa awali hivyo kwa yoyote anaeweza kunisadia naomba ajitokeze " amesema Mambeta.
 


Amesema kuwa anaomba wadau kumchangia kupitia nambari hii 0714435312 ili aweze kujikwamua katika changamoto mbalimbali za kimaisha.
 


Pia alitoa wito kwa wapenzi na wanachama wa CCM kujitokeza kumsadia kwani wao ni moja ya watu waliokuwa wahamasishaji wakubwa kupitia TANU mpaka ilipozaliwa CCM walitumia mpira kama sehemu ya hamasa.


 Wachezaji wa zamani wakiongozwa na Kitwana Manara wakimjulia hali, Athur Mwambeta,ambaye amekatwa miguu yote miwili

LESSONS FROM SOCCER

LESSONS FROM SOCCER

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Article by: Allan Lucky
When defenders & goalkeepers work so hard to ensure clean sheets, when midfielders put in lots of effort to ensure balls are ready for delivery, when wingers provide enough crosses and strikers/forwards make sure balls get at the back of the net - the team wins.
It applies in real life. Most people fail because there's no 'team-work'. There's no one-man show, never happened in the history of man-kind. Anyway, what surprises me most isthat some of us are soccer fans but don’t learn. We have goalkeepers and defenders in real life. These are the people whom we all turn to whenever things go south. 
We depend on them to defend us or ensure we do not fall or fail. They may be in your family, circle of friends or relatives. Some could also be in your office or area of expertise. Trust them, they will definitely defend and ensure you get a clean sheet in whatever project/activity you get involved in.
We have midfielders and wingers in real life. Like the defenders, they are available at home, school, work or in the community. They readily avail resources for you to grab/embrace and use to your own advantage and progress. These are support systems that are around. 
We have people helping us with finances, skills, connections, etc. Systems are in place to ensure we excel in life at all angles - schools/learning institutions, business centers, churches/mosques, etc. These midfielders and wingers in life ensure everything is ready for you to score, get the three points and move up the table.
You are the striker, you are the forward. The team will not win even if defenders/goalkeepers record another clean sheet.  Midfielders and wingers prepare everything for you - yet you do not score. You are a striker/forward of your life. You are a striker/forward of your own career. You are required to kick that final ball in a fashionable way to ensure the victory. If it's a header, even better! 
Remember, if you win, it's not only your victory, but your team's victory. From now on, start thinking of your team members. Ask yourself: Who is my defender? Who's my winger? Most importantly, appreciate everyone who kicked the ball before you got that 'little beauty' on target. And most importantly, do not ever lose the ball in your opponent's 18-yard box. 
All the efforts and work put in by others will be in vain. You will lose the game, lose your career and definitely lose your life. Note that you can also play different positions when things get tough, just like at times you see Wayne Rooney defending. Another determinant is the formation of the game, in this case the formation of your life and career. 
You can play different positions for someone else’s team/game. Remember, as others ensure that you become a striker of your team, you too have a role of making them strikers of their respective teams by being their defender, winger and midfielder.  
Now, STRIKE WHILE THE IRON IS HOT!
That's all for now folks!
Mob: +254724805536

E-mail: alpalogix@gmail.com

Zlatan Ibrahimovic alivyo tembelea sanamu linalotengenezwa kwa ajili yake

Zlatan Ibrahimovic alivyo tembelea sanamu linalotengenezwa kwa ajili yake

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Zlatan Ibrahimovic alipotembelea kuona sanamu hilo. Sanamu hilo ambalo litawekwa kwenye sehemu maalum katika mji wa Stockholm nchini Sweden. Zlatan amekuwa na mchango mkubwa na hamasa katika soka la nchini hiyo.
Kwa sasa ni mchezaji wa Man United lakini akiwa amepata mafanikio makubwa kutoka katika timu mbalimbali zikiwemo Ajax, Inter Milan, AC Milan, Juventus na FC Barcelona.

Bongo5

Arsenal yachambuliwa kama Karanga na Everton usiku wa jana

Arsenal yachambuliwa kama Karanga na Everton usiku wa jana

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Arsenal wamepoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya Everton kutoka nyuma na kuondoka na ushindi wa 2-1.


Washika bunduki hao walishinda michezo mitatu mfululizo walianza vyema katika mchezo dhidi ya Everton baada ya Alexis Sanchez kupiga safi mkwaju wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari uliombabatiza mlinzi Ashley Williams na kuingia wavuni.
Everton walisawazisha na kuwa dakika chache kabla ya kwenda mapumzikoni baada ya Seamus Coleman kumalizia vyema mpira uliopigwa na mlinzi Leighton Baines.
Kipindi cha pili kila timu ilirejea kwa lengo la kuchukua alama tatu lakini ni Everton ndio waliofanikiwa baada ya Williams kufuta makosa yake kwa kuifungia Everton goli la pili na la ushindi.
Nahodha wa timu ya Everton Phil Jagielka alitolewa kwa kadi nyekundu dakika chache tu kabla ya kumalizika kwa mchezo huo baada kupata kadi ya pili ya njano. Kwa matokeo hayo Arsenal wanabaki nafasi ya pili wakiwa na alama 34 wakiwa mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya vinara Chelsea wenye alama 37. Everton wanabakia nafasi ya saba wakiwa na alama 23.

Jermain Defoe afikisha idadi ya mabao 150

Jermain Defoe afikisha idadi ya mabao 150

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mchezaji wa klabu ya Sunderland, Jermain Defoe ameungana na watabe wengine wa soka ambao wamefikisha idadi ya mabao 150 kwenye historia ya mashindano ya ligi kuu England.

Siku ya November 19 Defoe amekuwa ni mchezaji wa 8 kuungana na wengine kwenye historia hii mara baada ya kuifungia klabu yake ya Sunderland FC bao moja kwenye ushindi wa mabao 3 dhidi ya klabu ya Hull City.

Chanzo: Bongo 5

Chelsea yamnasa Batshuayi

Chelsea yamnasa Batshuayi

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Klabu ya Chelsea imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji aliyekuwa anaichezea Marseille Michy Batshuayi kwa £33m.

Kuanzia msimu ujao Chelsea itaanza kunolewa na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Italia katika michuano ya Euro 2016 Antonio Conte.


Batshuayi mwenye umri wa miaka 22, amesaini mkataba wa miaka mitano ya ndani ya Stamford Bridge London England.

Wales and England zimetinga hatua ya Mtoano Euro 2016

Wales and England zimetinga hatua ya Mtoano Euro 2016

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Michuano ya Euro 2016 imeendelea June 20 kwa michezo miwili ya Kundi B kuchezwa,Slovakia alicheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B dhidi ya England na kumalizika kwa sare ya 0-0, matokeo ambayo yameifanya England kutinga hatua ya mtoano.
QWQWQ
Kwa upande wa Wales imefanikiwa kuifunga Urusi kwa Jumla ya goli 3-0, hivyo hizo zinaweza kuwa habari njema kwa mashabiki wa Euro 2016 kuona Urusi yenye mashabiki wenye fujo inatolewa katika mashindano hayo, Magoli ya Wales yalifungwa na Aaron Ramsey dakika ya 11, Neil Taylor dakika ya 20 na Gareth Bale dakika ya 67.

Haya ndio maelezo ya Puma kuhusu ubora wa jezi walizotumia Uswiss dhidi ya Ufaransa

Haya ndio maelezo ya Puma kuhusu ubora wa jezi walizotumia Uswiss dhidi ya Ufaransa

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Siku sita za Samuel Eto’o na mkewe wakienjoy ndani ya ndoa yao, iko hivi

Siku sita za Samuel Eto’o na mkewe wakienjoy ndani ya ndoa yao, iko hivi

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
3

Mtu wangu wa nguvu naomba nikuletee picha tatu za Samuel Eto’o siku sita baada ya kufunga ndoa, akiwa na mke wake Georgette Tra Lou katika mapumziko yao ya ndoa na wakati huu ambao Ligi za Ulaya zimemalizika.
2

Huu ndio Msimamo wa Kundi A, Romania ikiaga Euro 2016

Huu ndio Msimamo wa Kundi A, Romania ikiaga Euro 2016

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
RAMAA


Romania walicheza mchezo wao wa kumamilisha ratiba dhidi ya vibonde wenzaoAlbania, ambapo katika mchezo huo Albania alifanikiwa kuibuka na ushindi wa kwanza na pekee katika mechi zake tatu za Euro 2016 na kuondoka na point tatu, baada ya kuifunga Romania goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Armando Sadiku dakika ya 43.

Hii ndio TOP 10 ya Red Cards zilizotolewa kimakosa

Hii ndio TOP 10 ya Red Cards zilizotolewa kimakosa

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Kosa moja katika soka linaweza kuigahrimu timu, nidhamu kujicontrol na hasira ni kitu ambacho kimekuwa kikitokea katika mchezo na wachezaji wajanja wajanja hutumia madhaifu au uzembe wa reaction ndogo za wachezaji wa timu pinzani kumshawishi refa kutoa kadi hata kama sio halali. TOP 10 ya kadi nyekundu zilizotolewa kimakosa

Ureno inahitaji kuifunga Hungary ili kusonga

Ureno inahitaji kuifunga Hungary ili kusonga

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Kama ni mpenzi wa michuano ya Euro 2016, usisahau kuwa kuna michezo mitatu imechezwa June 18 2016, moja kati ya mchezo uliochezwa usiku wa June 18 ni mchezo kati ya Ureno dhidi ya Austria, huu ulikuwa ni mchezo ambao Ureno na  Austria zote zilikuwa zinahitaji ushindi.
ro1
Cristiano Ronaldo ambaye ndio nahodha wa Ureno, alishindwa kuiongoza timu yake iibuke na ushindi dhidi ya Austria na matokeo yake wakaambulia sare ya pili mfululizo katika mchezo wao wa pili wa Kundi F, mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 0-0,wakati nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo tulishuhudia akikosa penati dakika ya 79.
ro 4
Msimamo wa Kund F
Kwa matokeo hayo maisha ya timu ya taifa ya Ureno kuendelea kusalia katika michuano ya Euro 2016, ni kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi F dhidi ya Hungary wanaoongoza msimamo wa Kundi hilo kwa kuwa na jumla ya point nne na Ureno wakisalia nafasi ya tatu nyuma ya Iceland.
ro
Mwisho wa mchezo huo shabiki alivamia uwanja na kukimbilia kupiga self naCristiano Ronaldo

Je wajua kwamba kwa zaidi ya miaka 15, Sweden haijawahi kuifunga Italia?

Je wajua kwamba kwa zaidi ya miaka 15, Sweden haijawahi kuifunga Italia?

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
bn
Msimamo wa Kundi E ulivyo baada ya matokeo ya mechi hiyo
Lakini kwa upande wa Sweden mara ya mwisho kupata ushindi dhidi ya Italia ilikuwa June 2 1998 katika mchezo wa kirafiki, lakini katika mchezo wa kimashindano Sweden iliifunga Italia Jun 3 1987 ulikuwa mchezo wa European Championship.

#Euro2016 Match Preview: Leo ni Vita ya kundi E, Italy vs Sweden

#Euro2016 Match Preview: Leo ni Vita ya kundi E, Italy vs Sweden

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Italy leo wanawania ushindi wa pili ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro pale watakapokuwa na kibarua kigumu mbele ya Sweden, katika mchezo wa kundi E utakaofanyika kwenye uwanja wa Stade  de Toulouse uliopo manispaa ya manispaa ya Tolouse majira ya saa 10 jioni.
Italy maarufu kama Azzurri walionesha ukomavu wake katika mchezo wa awali uliochezwa Jumatatu dhidi ya Ubelgiji baada ya kushinda mabao 2-0, magoli yaliyofungwa na Emanuele Giaccherini na Graziano Pelle licha ya muda mwingi kuelemewa na wapinzani wao.
Ushindi wa leo utawafanya vijana hao wa Antonio Conte kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano na kuwasubiri wapinzani wao wengine watakaokuwa wakiwania nafasi ya kuungana nao.
“Nadhani nina kundi la wachezaji wenye akili nyingi mno katika kikosi changu, wengi wao wana hamu ya kuona tunafanya kitu chenye tija, na ndio maana tunapambana kuhakikisha tunavuka hatua hii ya makundi.” amesema Conte.
“Wanafahamu fika kwamba, tunapaswa kupambana kwa asilimia 100, kwasababu kama tuncheza kwa kiwango cha kawaida, tafsiri yake hatuwezi kupata matokeo. Ni lazima tufanye kitu cha ziad ili kuwafanya mashabiki wetu wajivunie timu yao.”
Kwa upande wa Sweden walianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland, walipata goli dakika ya 71, goli ambalo Jamhuri ya Ireland walijifunga wenyewe.
Macho yote kwa siku ya leo tena yatakuwa kwa nahodha wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ambaya anasaka kuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye michuano minne mfululizo ya Ulaya na kumzidi Cristiano Ronaldo baada ya kushindwa kuonesha uwezo wake kwenye mchezo wa kwanza.
Lakini kocha wa Sweden Erik Hamren amemtetea nahodha wake huyo na kuwaasa wachezaji wake wote kwa umoja wao kucheza kwa badii kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi.
“Ili kuwa mshambuliaji bora, lazima upata sapoti kwa wachezaji wenzako. Safu yetu ya ushambuliaji haikuwa katika ubora unaohitajika. Ndani ya dakika 50 za mwanzo washambuliaji wetu hawakuwa wakipewa huduma nzuri.”amesema Hamren
“Tulianza kuingia mchezoni taratibu na kuanza kutengeneza nafasi. Ibrahimovic alihusika kwenye lile goli. Tunatakiwa kujitolea kwa asilimia 300 kwenye mechi zijazo kama tunataka kushinda.”
Takwimu muhimu kuelekea mchezo wa leo
Italy
  • Magoli saba kati ya tisa ya mwisho ya Italy dhidi ya Sweden yamefungwa katika kipindi cha kwanza.
  • Chini ya Antonio Conte, Italy hawajafungwa mechi 11 za ushindani (ushindi mara 8, droo tatu). Kipigo chao cha mwisho kilikuwa dhidi ya Uruguay wakati wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 (wakati huo ikiwa chini ya Cesare Prandelli)
  • Katika michezo ya mwisho 34 ya michuano ya Ulaya, Italy hawajafunga zaidi ya magoli mawili.
  • Katika michezo yao 3 ya mwisho, Italy wamecha bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa.
  • Italy wamepoteza michezo miwili tu kati ya 22 katika hatua ya makundi ya fanali za michuano ya Ulaya (wameshinda mara 11, sare mara 9)
  • Antonio Candreva amehusika katika magoli matatu katika michezo miwili iliyopita kwa Italy (amefunga goli moja na kutoa assist mbili)
Sweden
  • Sweden wameshinda michezo yao mitatu tu kati ya 15 katika michuano ya Ulaya (sare 5 na kufungwa mara saba).
  • Licha ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland, Sweden hawakupiga hata shuti moja lililolenga lango.
  • Zlatan Ibrahimovic anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mara nne katika michuano minne tofauti ya Ulaya kama atafunga leo. Mpaka sasa ana magoli sita katika michezo 11, ukijumlisha na ule dhidi ya Italy mwaka 2004.
  • Magoli saba ya mwisho ya Sweden yamefungwa na wachezaji saba tofauti (liliwemo moja la kujifunga).

Fainali ya tano, Poland haijawahi kuifunga Ujerumani

Fainali ya tano, Poland haijawahi kuifunga Ujerumani

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Michuano ya Euro 2016 imeendelea kama kawaida June 16 2016, michuano inazidi kuwa migumu kutokana na timu kuingia katika round ya pili ya hatua ya Makundi, hivyo zinahitaji point ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi, June 16 imechezwa michezo mitatu, lakini mchezo kati ya Ujerumani dhidi ya Poland ulionekana kuwa mgumu zaidi.
Katika mchezo wa Ujerumani dhidi ya Poland umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 0-0, hivyo kutokana na timu hizo michezo yao ya kwanza ilipata ushindi, zote zinakuwa zimetimiza point nne ila Ujerumani anaongoza Kundi C kwa tofauti ya magoli, wakati Ukraine kutokana na kutokuwa na point hata moja, wanasubiri kukamilisha ratiba.
qwerty
Baada ya matokeo hayo hii inakuwa fainali ya tano kubwa kwa timu ya taifa ya Poland kushindwa kupata ushindi mbele ya timu ya taifa ya Ujerumani, Mario Gotze na Mesut Ozil walionekana kupata nafasi amabazo wangeweza kuipatia ushindi Ujerumani, ila golikipa wa Poland Lukasz Fabianski alionekana kuwa imara kwa kuokoa hatari zote golini.

MICHUANO YA COPA AMERICA YAFIKIA ROBO FAINALI

MICHUANO YA COPA AMERICA YAFIKIA ROBO FAINALI

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com



Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

 MICHUANO ya Copa America inayoonekana moja kwa moja kupitia visimbuzi vya StarTimes Tanzania imefikia hatua ya robo fainali ambayo itaanza kutimua vumbi kesho Juni 16 mpaka 19.

Timu zilizotinga hatua hiyo ni Argentina, Chile, Mexico, Marekani, Venezuela, Peru, Colombia na Ecuador huku mashabiki wa soka wakishuhudia miamba ya soka ya timu za Brazil na Uruguay wenye nyota lukuki kama vile Luis Suarez, Edinson Cavani, Willian, Countinho na wengineo wakishindwa kuzisaidia timu zao.

Katika michuano hii ya kusisimua kikosi cha timu ya taifa cha Argentina kikiongozwa na mchezaji bora wa dunia mara tano, Lionel Messi, ambacho kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo kimeingia kwa kishindo hatua ya robo fainali baada kushinda michezo yote mitatu na kuongoza kundi D kwa alama tisa.

Kupitia chaneli za Sports Focus na World Football wateja na watanzania wanatazama michezo yote moja kwa moja huku wakiwa na nafasi ya kusinda zawadi mbalimbali kama vile vifurushi vya bure pamoja na pesa taslimu na safari kwenda Ujerumani kutazama mechi za Bundesliga za msimu ujao unaotarajiwa kuanza mwezi wa nane.

Akitoa ufafanuzi juu ya michuano hiyo Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa, “Mbali na kufurahia matangazo ya moja kwa moja ya mechi zinazochezwa nchini Marekani pia tuna kampeni inayoendelea ya ‘Tabiri na Ushinde’ inayoenedelea kupitia mitandao yetu ya facebook na instagram.

Kupitia kampeni hiyo mteja anaebashiri kwa usahihi matokeo ya mechi ya siku husika hupata fursa ya kujishindia kifurushi cha Mambo pamoja na cha michezo cha Sports Plus cha jumla ya shilingi 36,000/-.”

“Mbali na hapo pia kuna zawadi zingine zinazotokana na kampeni ya hashtag ya #CopaAmericaonStarTimes kupitia mitandao yetu pia. Mshindi wa kampeni hii hupatikana kwa kushea mara nyingi zaidi post atakayoiona kuwekwa na kurasa za StarTimes na kufikia watu wengi zaidi. 

Mshindi wa kwanza wa kampeni atapatiwa tiketi VIP ya kwenda ya kwenda Ujerumani kutazama mechi za Bundesliga msimu ujao pamoja na dola za Kimarekani 1500/-, huku wa pili na wa tatu watapatiwa simu za mkononi za kisasa aina ya Solar 5. Tumefanya hivi ili kuwazawadia wateja wetu waaminifu na wanaofuatilia huduma zetu ili kunogesha zaidi shamra shamra za kombe la Copa America.” Alimalizia Bi. Hanif 

Hatua ya robo fainali itakayoanza kupigwa kesho itazijumuisha timu zote zilizoshika nafasi ya pili katika makundi yao.  Wapenzi wa soka ulimwenguni wanazidi kusononeshwa na mwenedo mbovu wa kikosi cha taifa cha Brazil ambacho kimeshindwa kutinga hatua hiyo kwa kufanikiwa kushinda mechi moja tu kati ya tatu. 

Matokea hayo mabovu yamepelekea kocha wa taifa timu hiyo Dunga kutimuliwa kazi.

Timu na ratiba kwa timu zitakazopambana ni  pamoja na Marekani na Ecuador (Juni 16), Peru na Colombia (Juni 17), na mechi za mwisho ni Argentina na Venezuela; Mexico na Chile (Juni 18). Timu zitakazopita hatua hii zitakutana katika hatua ya nusu fainali siku ya Juni 21.

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .