Wales and England zimetinga hatua ya Mtoano Euro 2016
Posted in
Michezo
No comments
Tuesday, June 21, 2016
By
danielmjema.blogspot.com

Michuano ya Euro 2016 imeendelea June 20 kwa michezo miwili ya Kundi B kuchezwa,Slovakia alicheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B dhidi ya England na kumalizika kwa sare ya 0-0, matokeo ambayo yameifanya England kutinga hatua ya mtoano.

Kwa upande wa Wales imefanikiwa kuifunga Urusi kwa Jumla ya goli 3-0, hivyo hizo zinaweza kuwa habari njema kwa mashabiki wa Euro 2016 kuona Urusi yenye mashabiki wenye fujo inatolewa katika mashindano hayo, Magoli ya Wales yalifungwa na Aaron Ramsey dakika ya 11, Neil Taylor dakika ya 20 na Gareth Bale dakika ya 67.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :