YOKOHAMA F-MARINOS YAITANDIKA MAN UNITED 3-2

Posted in
No comments
Tuesday, July 23, 2013 By danielmjema.blogspot.com

MANCHESTER UNITED leo wameanza Ziara yao huko Japan kwa kichapo cha Bao 3-2 toka kwa Yokohama F-Marinos katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Kimataifa wa Yokohama.

Hiki ni kipigo cha pili kwa Man United katika Ziara yao huko Asia ambako walianza kwa kufungwa Bao 1-0 huko Bangkok, Thailand na Singha All-Stars Wiki iliyopita kisha Jumamosi iliyopita wakashinda Bao 5-1 huko Sydney, Australia walipoichapa A-League All Stars.

MAGOLI:
Yokohama F-Marinos 3
-Marquinhos Dakika ya 1
-Fabio Aguiar 49
-Fujita 87
Manchester United 2
-Lingard Dakika ya 19
-Tashiro 31 [Kajifunga mwenyewe]

Mechi inayofuata kwa Man United ni Ijumaa Julai 26 huko Osaka watakapocheza na Cerezo Osaka, Klabu ambayo Mchezaji wa Man United Shinji Kagawa alikoanzia Soka.

KIKOSI CHA MAN UNITED KILICHOANZA:

De Gea; Fabio, Jones, Evans, Evra, Anderson, Cleverley, Lingard, Zaha, Januzaj, Van Persie
Akiba: Amos, Rafael, Smalling, Buttner, Keane, Giggs, Young, Kagawa, Welbeck

KIKOSI CHA MAN UNITED KWENYE ZIARA:
MAKIPA: David de Gea, Anders Lindegaard, Ben Amos

MABEKI: Rio Ferdinand, Jonny Evans, Phil Jones, Michael Keane, Rafael, Fabio, Alexander Buttner, Patrice Evra, Chris Smalling

VIUNGO: Michael Carrick, Tom Cleverley, Anderson, Ryan Giggs, Wilfried Zaha, Jesse Lingard, Adnan Januzaj, Shinji Kagawa, Ashley Young

MAFOWADI: Danny Welbeck, Robin van Persie

MANCHESTER UNITED==ZIARA:


Julai 13 Singha All Star 1 Man United 0
Julai 20 A-League All Stars 1 Man United 5
Julai 23 Yokohama F-Marinos 3 Man United 2
Julai 26 Cerezo Osaka (Osaka Nagai Stadium, Osaka) [Saa 7 Mchana]
Julai 29 Kitchee (Hong Kong Stadium, Hong Kong) [Saa 9 Mchana]
Agosti 6 AIK Fotboll (Friends Arena, Stockholm)
Agosti 9 Sevilla (Old Trafford - Rio Ferdinand Testimonial)

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .