MUUGUZI AMKATAKATA MAPANGA MFANYAKAZI WAKE WA NDANI-SAME-KILIMANJARO

Posted in
No comments
Sunday, May 19, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Na Kija Elias, Same

http://cdn1.blovcdn.com/bloglovin/3a945e0d2df75f6d1d1f7f8505ea5ad02517e230/d/aHR0cCUzQSUyRiUyRjQuYnAuYmxvZ3Nwb3QuY29tJTJGLUJhbHNDdkl6RVpBJTJGVGdDQWM3MUFWaEklMkZBQUFBQUFBQUFPOCUyRngxU0hMQzFkVFFJJTJGczMyMCUyRmNyeS5qcGc=
Mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Restuta Luawilo (19), ambaye ni mfanyakazi wa ndani amewalazwa katika ya hospitali ya wilaya ya Same akiuguza majeraha baada ya kufanyiwa kitendo cha ukatili na mwajiri wake.

Akiongea kwa uchungu akiwa kitandani hospitalini hapo, Luawilo alisema kuwa kitendo hicho cha kinyama alifanyiwa na mwajiri wake aliyemtaja kwa jina la Joyce Shemahonga, ambaye ni muuguzi wa kituo cha Afya cha Tumaini. Luawilo ambaye amelazwa katika hospitali hiyo, alisema mwajiri wake huyo alimfanyia unyama huo siku ya Jumapili iliyopita kuanzia majira ya saa mbili usiku hadi saa nane za usiku.  

Akizungumza hospitalini hapo, Luawilo alisdema kuwa chanzo cha kufanyiwa unyama huo ni kukumbushia mshahara wake ambayo amekuwa akidai kwa muda mrefu.

Alisema kuwa baada ya kutokea kutoelewana kati yao, mama huyo akishirikiana na mume wake aliyemtaja kwa jina moja la Abel, ambaye ni mwalimu walimkata na kumfunga miguu na mikono kwenye kitanda ili asiweze kutoka kwa madai ya kumuibia shilingi milioni mbili, wakafunga mlango na kuondoka. 

Alisema kuwa waajiri wake walitumia nondo kumpiga nayo maeneo mbalimbali ya mwili kabla ya kumfunika na kitambaa usoni na kuanza kumkatakata na kuongeza kuwa mume wa mama huyo alikuwa anatumia panga huku mama akitumia kisu na kumlazimisha aseme alikoweka fedha zao. 

 “Walitumia nondo kunipiga nayo maeneo mbalimbali ya mwili wangu na kasha wakanifunika kitambaa usoni na kuanza kunikatakata, mume akitumia panga na mama akitumia kisu huku wakinilazimisha niseme fedha ziko wapi”, alisema. 

Luawilo alisema baada ya maumivu makali alianza kulia na majirani waliposikia wakaenda kutoa taarifa polisi ndipo wakaja na kwa kushirikiana na majirani wakanipeleka hospitali. 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi, aliyefika hospitalini hapo kumtembelea binti huyo, aliagiza mama huyo na mumewe wakamatwe mara moja na kuongeza kuwa kitendo kama hicho siyo cha kuvumilika kabisa. 

Mmoja wa majirani aliyekwenda kutoa taarifa polisi Jenifer Stanley, alisema kuwa walisikia binti huyo akipigwa usiku huo na kwamba hawakuchukulia maanani kwa vile illikuwa ni jambo la kawaida mama huyo kumpiga binti huyo mara kwa mara. 

“Baadae binti huyu alikuja usiku wa manane nyumbani kwangu baada ya kupata mwanya na kutoroka huku akiwa anavuja damu mwilini lakini tukashindwa kumsaidia kutokana na hali yake kuwa mbaya na ndipo asubuhi tukaenda kutoa taarifa kesho yake, (Jumatatu 13/5/2013)”, alisema.
 
Source: Zanzibar Leo

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .