BOHARI YA DAWA (msd) YAAGIZA VITUO VYA AFYA KUFIKISHA DAWA MAPEMA SEHEMU HUSIKA KUDHIBITI WIZI WA DAWA..........

Posted in
No comments
Tuesday, May 21, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Washiriki wa semina elekezi kwa wadayu wa afya kutoka katika vituo vya afya mbalimbali nchini kuhusu namna ya kupambana na tatizo la wizi wa madawa katika vituo vya afya na mahospitali iliyoandaliwa na Bohari kuu ya Madawa Tanzania (MSD), jana katika Hoteli ya Naura Spring jijini Arusha.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi, (aliyevaa shati la kijivu) akifuatilia kwa makini maelekezo katika Semina elekezi juu ya namna ya kudhibiti wizi madawa katika vituo vya afya pamoja na athari zake za wizi huo kwa jamii
Meneja wa Bohari ya Dawa kanda ya Moshi, Dkt. Celestine Haule akitoa maelezo kwa washiriki kuhusu njia za kudhibiti wizi wa dawa unaotokana na ucheleweshwaji wa dawa katika sehemu husika
Washiriki wa semina hiyo kutoka katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara katika picha ya pamoja, Hoteli ya Naura Spring jijini Arusha

Mwandishi Wetu, Arusha

Hospitali zote zilizopo katika Kanda ya Tanga na Moshi zimeagizwa kufikisha dawa kwa wakati,vifaa tiba na vitendanishi, hadi ngazi ya zahanati, lengo likiwa ni kupunguza malalamiko yaliyopo kwa wagonjwa ya kutokuwepo kwa vifaa hivyo katika vituo vya kutolea huduma.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa bohari ya dawa kanda ya Moshi Celestine Haule wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa MSD ulio jumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha wenye lengo la kuingiza mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kuhusu zoezi la upelekaji wa dawa moja kwa moja kwa wateja wao.

Haule alisema kuwa Hospitali nyingi hapa nchi zimekuwa hazichukui dawa hali ambayo imechangia dawa nyingi kumaliza muda wake huku wagonjwa wakikosa dawa pindi wanapokwenda kupata huduma hiyo.

Alisema endapo hospitali zitaweza kufikisha haraka dawa katika zahanati zilizoko vijijini zitaweza kutatua changamoto hizo na hivyo kupunguza malalamiko kwa kiasi kikubwa kwa wagonjwa.

“Ninaziagiza hospitali zote hapa nchini kusambaza dawa hadi ngazi ya chini katika zahanati zetu, dawa hizi zikifikishwa kwa wakati na kiwango kilichoagizwa tutaweza kutatua changamoto hizi zilizopo”, alisema Haule.

Hata hivo Haule alifafanua kuwa upatikanaji wa dawa kwa sasa umeongezeka na kufikia  asilimia 85 kutoka asilimia 30 iliyokuwepo kabla ya zoezi upelekaji wa dawa moja kwa moja kwa .      

Akifungua mkutano huo Kaimu Mkurugenzi  wa MSD amesema mikakati ya MSD ni kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kufikisha dawa hadi ngazi ya zahanati na hospitali za mikoa yote ifikapo Julai 2013.

Alisema ili tuweze kuwahudumia kwa kiwango kizuri tunahitaji hospitali zote kuwasilisha mahitaji yake ndani ya siku kumi na nne kwa MSD ili tuweze kujiaandaa vya kutosha kuhakikisha oda zilizoombwa zinakamilika kwa wakati.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .