OBAMA KUTUA TANZANIA JUNE 2013.
Posted in
No comments
Wednesday, May 22, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuzuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania mwezi Juni. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya White house.
Rais Obama atakutana na watunga sheria na wafanyabiashara pamoja na viongozi wa asasi za kijamii.
Ziara ya Obama itaanza tarehe 26 Juni hadi 3 Julai na itakuwa ziara yake
ya pili Kusini mwa jagwa la Sahara akiwa rais wa Marekani. Aizuru Ghana
mwaka 2009
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na mwenzake George W Bush, wote
walizuru Afrika wakati wa muhula wao wa pili wa utawala. Clinton alizuru
nchi sita wakati Bush Alizuru nchi tano
''Rais atatilia mkazo uhusiano kati ya Marekani na baadhi ya nchi za
kiafrika ambazo zinakuwa ikiwemo maswala kama ukuwaji wa uchumi,
uekezaji na biashara pamoja na kukuza taasisi za kidemokrasia na
kuendelea kukuza viongozi wa kizazi kijacho Afrika,'' ilinukuu taarifa
kutoka ikulu ya White House.
Rais Barack Hussein OBama wa Marekani akiwa na Bibi yake alipozuru Kenya. |
Ziara ya Obama pia itatilia mkazo kukuza uhusiano kati ya Marekani na
watu wa bara la Afrika ili kuendeleza ushirikiano wa kikanda, amani na
ukuwaji.
Wadadisi wanasema kuwa ziara kama hizi hufanywa sana na marais wa
Marekani hasa baada ya kuondokewa na kazi ngumu ya kampeini za uchaguzi
na shinikizo za ndani ya nchi.
Wakati huohuo, tisho linaloongezeka kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu
nchini Mali, limefanya kanda hiyo kumulikwa zaidi na Marekani. Bi Michel
Obama ataambatana na mumewe katika ziara hiyo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :