BREAKING NEWS: BAADA YA YANGA, TUSKER NAYO YATANGAZA KUJITOA KOMBE LA KAGAME

Posted in
No comments
Thursday, June 13, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Wakati Yanga imetangaza kujitoa katika michuano ya Kagame Cup, mabingwa wa Kenya, Tusker nao wametangaza kujiondoa. Kwa mujibu wa mtandao wa SuperSport wa Afrika Kusini, Tusker pia imejitoa kutokana na kutokuwa na uhakika kuhusiana na usalama kwa kuwa moja ya miji itakayofanyika michuano hiyo ni Darfur. Mmoja wa maofisa wa Tusker, Charles Obiny ameiambia SuperSport kwamba wameamua kujitoa kutokana na kutokuwa na uhakika wa usalama nchini Sudan. 

 “Haukuwa uamuzi lahisi, lakini baada ya mjadala wa kutosha, tumeamua kujitoa mara moja kwa kuwa hata waandaaji (Cecafa) wameonekana kushindwa kuthibitisha usalama. Hivyo tunafanya hivyo kwa wachezaji wetu,” alisema Charles Obiny. Tusker imekuwa timu ya pili kujitoa baada ya Yanga ya Tanzania huku Simba na Falcon za Zanzibar nazo zikielezwa 


AWALI....
 

YANGA YAJIVUA UBINGWA WA KOMBE LA KAGAME, CECAFA YAWAPA WAGANDA NAFASI YAKE



Mabingwa watetezi mara mbili wa michuano ya Kombe la Kagame, Yanga wametangaza kujiondoa kushiriki michuano hiyo.

Kupitia mtandao wake, Yanga imethibitisha kujitoa katika michuano hiyo ambayo kama wangeshinda wangekuwa wamebeba kombe mara ya tatu mfululizo.

Maana yake baada ya kushinda kombe hilo mara mbili mfululizo, Yanga imeamua kujivua ubingwa.

Michuano hiyo imepangwa kufanyika nchini Sudan na Yanga imechukua uamuzi huo kutokana na vigezo vya hofu ya kutokuwa na amani ya kutosha nchini humo.

Hofu kubwa ilikuwa ni katika jimbo la Darfur ambalo limekuwa na mapambano ya silaha mara kwa mara.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .