MANISPAA YA MOSHI YABOMOA NYUMBA KWA AGIZO LA BARAZA LA MADIWANI

Posted in
No comments
Thursday, July 4, 2013 By danielmjema.blogspot.com

MKURUGENZI wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro Bernadeta Kinabo,ametelekeze agizo la baraza la madiwani la kumtaka kuvunja nyumba iliyojengwa katika eneo la wazi bila kibali kuvunjwa.

Mfanyabiashara maarufu John Ambrose Mwasi akikagua baadhi ya vitu vyake baada ya Manispaa kubomoa Nyumba yake majira ya saa saba usiku kutekeleza agizo la baraza la madiwani

TAIFA LETU.com imefika katika eneo la tukio leo asubuhi na kushuhudia shughuli ya kuvunja nyumba hiyo ikiwa ikekwisha fanyika ambapo baadhi ya mashuhuda walisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 7:00 usiku.

Nyumba hiyo  inayolalamikiwa na madiwani hao kujengwa katika eneo la wazi ipo katika mtaa wa polisi mesi barabara ya mawezi karibu na makao makuu ya jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro.

Katika baraza la madiwani lililo kaa juzi katika ukumbi wa Manispaa mkurugenzi huyo alitakiwa kuvunja nyumba hiyo pamoja na baadhi ya nyumba nyingine zilizo jengwa kinyume cha sheria.

Diwani wa kata ya Kiusa Steven Ngasa alidai katika kikao hicho kuwa nyumba hiyo ilijengwa kinyume cha sheri na kwamba madiwani wamekuwa wakilaumiwa kuchukua rushwa kutoka kwa wamiliki hao jambo ambalo si kweli.
 
Alisema kuwa kumekuwa na ujenzi holela unaoendelea ndani ya manispaa hiyo huku watendaji wa Halmashauri hiyo wakiwa hawatambukii chochote kinacho endelea jambo ambalo ni uzembe.

“tabia hii ya ujenzi holela imekuwa ikishamiri siku hadi siku na mbaya zaidi wanakiuka sheria jambo hili hatuta livumili kuona linaendela katika manispaa yetu”Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manspaa  Kinabo alisema kuwa baadhi ya madiwa wamekuwa wakipita kwa wamiliki wa majengo hayo huku wakichukua rushwa jambo ambalo limekuwa likikwamisha shughuli hizo kuendelea.

Naye Meya wa manispaa hiyo Jafari Michael aliwataka madiwani kuacha tabia ya kuwa “mawakala wa nyumba” na kutanguliza maslahi mbele kwani wao ndio chanzo cha migororo inayo endelea ndani ya mansipaa hiyo.
 
Akizungumzia tukio la kuvunjiwa nyumba yake, mmiliki wa Nyumba hiyo, John Ambrose Mwase amesema hapo mwanzoni alikuwa anafanya biashara ya mgahawa katika eneo hilo kabla ya kuiomba manispaa imbadilishie leseni ya biashara na kibali cha kufanya biashara tofauti katika eneo hilo.

Amesema anashangazwa kusikia kuwa ujenzi wa nyumba hiyo umefanyika bila kibali na kuhoji ni kwa nini manispaa ichukue uamuzi wa kuvunja majira ya usiku na kuharibu mali bila taarifa.

Mwasi amesema leseni alipewa na Afisa biashara wa manispaa ambaye pia alifika na kukagua eneo hilo kabla ya ujenzi kuanza. ameongeza kuwa gharama ya mali zilizoharibika ni milioni 358 ambayo ni mkopo kutoka benki ya KCB.






Wananchi wakishangaa mali iliyoharibika kutokana na kitendo cha manispaa kubomoa nyumba ya Mfanyabiasha majira ya usiku




Mwasi akiwa ameshika Godoro
mpiga pich awa Mwananchi Dionis Nyato akipata maelezo kutoka kwa mmiliki wa Nyumba iliyobomolewa leo, majira ya saa saba usiku.

Wananchi wakiokota mabaki ya vitu vya thamani vilivyoteketezwa kjatika zoezi la bomoabomoa uliofanywa na Manispaa ya Moshi
Habari na picha na Kija Elias

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .