WANANCHI SAME KUNUFAIKA NA UPIMAJI WA VIWANJA VYA MAKAZI 3,000

Posted in
No comments
Wednesday, July 10, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akikabidhi kifaa cha upimaji kwa Christopher Ilila
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkabidhi kifaa cha upimaji Mwenyekiti wa Halmshauri ya Same, Christopher Ilila

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akikabidhia kifaa cha upimaji wa Ardhi kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Same, Christopher Ilila

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akijaribu kupima kwa kutumia kifaa kipya cha upimaji wa Ardhi

Mpima Ardhi wa Halmashauri, Hemedi Juma, ambaye ni mtaalamu wa Upimaji, akimuonesha Gama jinsi ya kupima kwa kutumia kifaa cha upimaji kilichonunuliwa kwa ajili ya kupima viwanja 3,000 wilayani Same, Mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjro Leonidas Gama, (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Same Herman Kapufi (kulia) na Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Christopher Ilila (picha zote na Kija Elias)
                                                                         ********
Wananchi wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro wanatarajia kunufaika na mpango wa kupima viwanja ambapo jumla ya viwanja 3,000 vya makazi vitapimwa wilayani hapo baada ya Halmashauri ya wilaya hiyo kununua vifaa vya upimaji Ardhi (Total station) kwa gharama ya shilingi milioni 38.

Akitoa taarifa ya mpango huo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, Mkurugenzi wa Wilaya ya Same, Joseph Mkude amesema kuwa katika mpango huo wakazi wa wilaya hiyo pia watanufaika na huduma nyinginezo.


Mkude amesema kuwa kwa kipindi kirefu Halmashauri hiyo ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa vifaa vya upimaji ardhi hali ambayo ilikuwa ikipelekea zoezi la upimaji wa Viwanja hivyo kushindwa kutekelezeka kwa wakatiuliopangwa.


Amesema kutokana na  uwepo wa vifaa hivyo, Halmashauri kwa sasa imelenga kupima viwanja 3,000 lengo likiwa ni kuweka mji vizuri na kwa mpango mzuri ili kila mwananchi aweze kunufaika.




Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .