RC-GAMA AKABIDHI GARI KWA HALMASHAURI YA SAME

Posted in
No comments
Wednesday, July 10, 2013 By danielmjema.blogspot.com

RC-Gama akifungua mlango wa Gari kuashiria uzinduzi, Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Same Herman Kapufi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama amekabidhi gari aina ya ana wakati wa makabidhiano wa Gari aina ya Hilux duoble cabin aliyoikabidhi kwa uongozi wa Halmashauri hiyo iliyonunuliwa kwa gharama ya shilingi 73.3 milioni.


katika makabidhiano hayo Gama amemtaka Mwenyekiti wa wilaya ya Same, Christopher Ilila kuiingia mkataba wa makabidhiano wa vifaa na watendaji wake wote ili kuwabana watumishi wabadhirifu.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro pia, amewataka viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Same kutumia gari hilo kwa manufaa ya wananchi na sio yao binafsi.

Amesema kuwa Gari hilo limetengwa kwa ajili ya kutumika katika idara ya fedha, kitengo cha mapato pamoja na kazi nyinginezo ili kuweza kuboresha shughuli za ukusanyaji wa mapato katika halmashauri hiyo lakini sio vibaya kama gari hilo litatumika kusaidia wananchi kwani wao ndio walengwa wakuu.



Aidha Gama ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kutafuta njia mbadala wa
kuongeza mapato katika Halmashauri huku akitahadharisha kuwashughulikia watumishi wabadhilifu ambao huingiza ubadhilifu
katika mradi huo.
(Habari zote na Kija Elias, Same)









Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .