Posted in
By
danielmjema.blogspot.com
Wanawake
wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza
shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8
nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na
Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika
wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward
ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa
miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika
Kusini.
Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya
uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka
watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Jumapili iliyopita NIPASHE ilipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za
kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika
Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku
ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika
Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na
takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’
zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh.
bilioni 6.8.
Mwanadada
huyu ambaye amejipatia umaarufu kutokana na 'kuuza sura' kwenye video
za mastaa mbalimbali wa muziki hapa Tanzania, Agnes Gerald (Agnes
Masogange) ni mmoja kati ya Wanawake wawili raia wa Tanzania
waliotambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya
zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini
wakitokea Tanzania.
0 MAOINI :