WILLIAM BURNS AKUTANA NA VIONGOZI MISRI.

Posted in
No comments
Tuesday, July 16, 2013 By danielmjema.blogspot.com

BURNS
Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani William Burns ambaye amefanya ziara nchini Misri, amelitaka jeshi la Misri na viongozi wa serikali ya muda, kuhakikisha kuwa mchakato wa kidemokrasia mnamo kipindi hiki cha mpito unashirikisha wote.

Burns ambaye ndiye afisa wa kwanza wa ngazi ya juu wa Marekani kuitembelea Misri tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyomwangusha rais Mohamed Morsi, amekanusha shutuma kuwa Marekani inaegemea upande mmoja katika mzozo wa kisiasa ulioigawa vibaya nchi ya Misri. 

Amefanya mazungumzo na rais wa mpito Adly Mansour, waziri mkuu mteule Hazem el-Beblawi,  na kamanda mkuu wa majeshi Jenerali Abdel-Fattah el Sisi. Maszungumzo hayo yalituama juu ya mpango mpya wa kidemokrasia uliopendekezwa na uongozi wa sasa.

 Mpango huo unataka katiba iliyoandikwa na vyama vya kiislamu chini ya utawala wa Morsi ifanyiwe mabadiliko, na kisha uchaguzi wa bunge na rais ufanyike mapema mwaka kesho. Hadi sasa udugu wa kiislamu umekataa katakata kushiriki katika mchakato wa sasa wa kisiasa, ukisema hautaki kuhalalisha mapinduzi yaliyomng'oa Morsi madarakani.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .