DAKTARI FEKI ANASWA KCMC

Posted in
No comments
Friday, September 6, 2013 By danielmjema.blogspot.com




Wagonjwa waliokuwa wanasubiri kupata huduma na watu wengine waliokuwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, jana walipata mshangao mkubwa baada ya uongozi wa hospitali hiyo kumnasa mtu aliyejifanya daktari wa watoto akiwa kwenye chumba cha upasuaji.
waandishi wa Habari wakimsikiliza afisa uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo (hayupo pichani)

Mtu huyo, Alex Sumni Massawe (33), alikamatwa saa 5:00 asubuhi ndani ya hospitali hiyo na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia, alikamatwa.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amepanga kufanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia huduma kwa malipo ya Sh. 200,000.

Habari zinasema kuwa kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana huyo, mkazi wa Manispaa ya Moshi, Pamvelina Shirima, alikutana na mtuhumiwa huyo katika baa moja maarufu mjini hapa iliyopo eneo la Dar Street (jina limehifadhiwa) na kumtaka ampe kiasi hicho cha fedha kwa madai zitatumika kuharakisha mwanaye wa kiume kufanyiwa vipimo vya upasuaji. 

Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo, alisema kuwa daktari huyo aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo baada ya baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mtu ambaye amekuwa akijitangaza kwamba ni daktari wa
“Huyu Alex Massawe tulimkamata leo (jana) asubuhi akiwa katika wodi ya upasuaji baada ya kupokea kiasi cha Shilingi 200,000 kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimleta mwanaye afanyiwe upasuaji wa ngozi.

Tunawataka wagonjwa wote kufuata taratibu ikiwamo kutokubali kurubuniwa na watu ambao hawajavaa sare wala kuwa na vitambulisho rasmi vya hospitali,” alisema Chisseo.


Alisema  kijana huyo alikuwa akihudhuria matibabu ya ngozi katika kliniki ya hospitalini hapo na kwamba madaktari hawakuona umuhimu wa kumfanyia upasuaji.
Alisema mtuhumiwa huyo alifanikiwa kupenya na kuingia wodini baada ya kutumia ujanja nje ya lango la kuingilia akijifanya na yeye ni
mgonjwa.


Uongozi wa KCMC ulipoulizwa kufafanua ilikuwaje mtuhumiwa huyo akaingia katika chumba cha upasuaji bila kuwa mfanyakazi wa hapo, ulisisitiza kuwa aliingia kwa kupenya.
Chisseo alisema mtuhumiwa huyo siyo  mwajiriwa wao na kwamba baada ya kuhojiwa alidai kuwa anafanya kazi katika hospitali hoja iliyoko Tabata, jijini Dar es Salaam.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alipotafutwa na TAIFA LETU.com kuzungumzia tukio hilo, alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye anajitambulisha kuwa ni daktari wa binadamu.Kamanda Boaz alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Katika siku za karibuni yametokea matukio kadhaa ya baadhi ya watu kukamatwa wakifanya kazi ambazo siyo taaluma zao.Baadhi yao wamekamatwa wakijiita maofisa usalama wa Taifa, polisi na askari wa usalama barabarani.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .