KINANA AWATAKA MAWAZIRI KUTATUA KERO ZA WANANCHI
Posted in
No comments
Tuesday, September 17, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka
mawaziri husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini
kushindwa kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza
kero za wananchi mitaji na kuwachajisha pesa nyingi hasa wafugaji.
Akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela alisema mawaziri
lazima wachukue jukumu la moja kwa moja kutatua matatizo ya wananchi,
alisema wafugaji wa kata ya Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu
wa hifadhi ya Maswa kupita kiasi, alisema sheria zingine ziangalia
wakati zinaweza zikawa zimepitwa na wakati hivyo ni vyema
zikarekebishwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kata ya Mwandoya ,kijiji cha Mandoya tarafa ya Kisesa ambapo Katibu Mkuu alipata maelezo ya utekelezaji wa ilani ya CCM. |
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Mwangesela wilayani Meatu mkoani Simiyu. |
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :