Breaking news:MABOMU YARINDIMA TAIFA MCHEZO WA SIMBA DHIDI YA KAGERA SUGER

Posted in
No comments
Thursday, October 31, 2013 By danielmjema.blogspot.com


Baada ya Kagera Suger kupata bao la kusawazisha dhidi ya Simba katika dakika ya 90 Polisi wamelazimika kutumia mabomu kutuliza ghasia baada ya mashabiki wa Simba kuanzisha vurugu katika uwanja wa taifa hivi sasa. 

Simba ilikuwa mbele kwa goli moja lililofungwa na Hamisi Tambwe katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza bao lililodumu hadi dakika ya 90 ya mchezo Kagera waliposawazisha kwa mkwaju wa penati na vurugu hizo kuanza.
Baada ya kupatikana kwa goli hilo, lililofungwa kwa mkwaju wa penati, mashabiki wa Simba walianza kufanya vurugu na kuvunja viti vilivyoko upande wa magharibi mwa uwanja kutokana na kutoridhika na maamuzi ya Mwamuzi wa mchezo jambo lililolazimu Jeshi la polisi la kutuliza Ghasia (FFU) kuingilia kati kupunguza madhara uwanjani hapo.




Polisi wakiwafuata mashabiki wa Simba ambao walikuwa wanang'oa viti

Simba sasa wanafikisha pointi 21 wakiendelea kukaa nyuma ya Azam FC,Mbeya City wenye pointi 23 na Yanga wenye pointi 22 huku Simba akicheza mchezo mmoja zaidi.
Mpaka viti vinavunjwa na mabomu yanaanza kupigwa Simba na Kagera walikuwa wamefungana bao 1-1.
Kagera ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Amisi Tambwe katika kipindi cha kwanza, walipata bao la kusaweazisha kupitia kwa Kanoni kwa njia ya panalti baada ya Joseph Owino kumwangusha Daudi Jumanne katika eneo la hatari.

 Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tabwe akimtoka beki wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. 
 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao.

 Mshambuliaji wa Kagera sugar, Temi Felix akimiliki mpira mbele ya beki wa Simba, Joseph Owino.
 Wachezaji wa simba wakiwa wameduwaa baada ya Kagera Sugar kupata penalti.
 Mashabiki wa Simba wakikanyagana baada ya kutokea vurugu kubwa katika jukwaa lao na kurusha viti uwanjani.
 Mashabiki wakitafutana baada ya Polisi kutumia mabomu ya machozi.
 Kila mtu akitafuta njia ya kutokea baada ya Polisi kutumia mabomu ya machozi kutuliza fujo zilizotokea katika jukwaa la Simba.
 Polisi wakimdhibiti shabiki aliyekuwa katika jukwaa la Simba.
 Viti vikiwa chini baada ya kung'olewa jukwaani.
 Polisi wakiondoka na shabiki wa Simba.
 Macho mbeleee.
 Hapa akijitetea kuwa si yeye aliyefanya fujo.
 Polisi hawakuwa na muda wa kumsikiliza.
 Jamani mnanionea bure.
 Sio mimi........
 Golikipa wa Simba, Abel Dhaira  akimlalamikia mwamuzi wa mchezo huo, Mohamed Theofile kutoka Morogoro.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .