BREAKING NEWS: DKT SENGONDO MVUNGI HATUNAYE TENA!!

Posted in
No comments
Tuesday, November 12, 2013 By danielmjema.blogspot.com


Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kutoka katika Hospitali ya Milpark ya Afrika Kusini zinaripoti kwa masikitiko makubwa kuwa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi Amefariki Dunai.

Taarifa hizo zilizosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zinadai kwamba Dkt. Mvungi alifariki dunia majira ya Saa 9:30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.



Dkt. Mugisha Clement Mazoko wa Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) (kushoto), Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (mwenye tai) na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia (wa pili kulia) pamoja na ndugu na jamaa wa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi wakiangalia wakati Mjumbe huyo akipandishwa ndani ya ndege leo kusafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Dkt. Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 3, 2013. (Picha na Tume ya Katiba)
Dkt. Mvungi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria katika chama cha NCCR-Mageuzi, alivamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumapili ya Novemba 3 mwaka huu, majira ya saa 7:30 usiku, nyumbani kwake katika eneo la Mpiji mpakani mwa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.



Kabla ya kukutwa na umauti huo, Dkt Mvungi alikuwa akipata matibabu Nchini Afrika Kusini katika Hospitali ya Milpark alikokimbizwa mnamo Novemba 7 mwaka huu baada ya hali yake kubadilika ghafla.

Mungu ilaze roho yake Mahali Pema Peponi!!

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .