MSAFARA WA RAIS KIKWETE WAPATA AJALI GEITA NA KUJERUHI WATU 5 WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI 3!!
Posted in
No comments
Tuesday, November 12, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Msafara wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya
Kikwete mkoani Geita, leo umeingia dosari baada ya gari moja
lilokuwa kwenye msafara huo kupinduka na kujeruhi watu watano.
Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja
wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.
|
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Geita
Lenard Paul ajali hiyo imetokea
leo saa 3 na dakika 45 asubuhi katika eneo la Nyankumbu kilomita 3 kutoka makao
makuu ya mkoa wa geita.
Kamanda
Paulo amesema gari hilo namba DFP.9730 aina ya Toyota Landcruzer lililokuwa
likiendeshwa Yungi Mkwati, mali ya Bohari kuu ya Madawa (MSD), lilipinduka
baada ya kuteleza kwenye lami iliyomwagwa barabarani hii leo.
Amewataja
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa
ni mwandishi Peter Makunga wa Radio Kahama Fm na Radio Free Afrika, Peter
Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick Katulanda Moderator wa Tovuti ya mabadiliko.com, meneja wa
MSD kanda ya Ziwa Byekwaso Tabura pamoja na dreva wa gari hilo Yungi Mkwati.
Kamanda
Paulo amesema majeruhi wote wamefikishwa katika hospitali ya wilaya ya Geita
kwa ajili ya matibabu na kisha kuruhusiwa huku Mwandishi Peter Makunga akiwa
bado amelazwa hospitalini hapo na hali yake inaendelea vizuri.
Mwandishi Peter Makunga akiwa anaendelea kupatiwa matibabu baada ya ajali hiyo, hospitali ya wilaya ya Geita. |
Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari. |
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :