DC MUHINGO: TAMASHA LA HANDENI NI FURSA YA MAENDELEO
Posted in
No comments
Tuesday, November 5, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Handeni
MKUU
wa
wilaya Handeni, DC Muhingo Rweyemamu, amewataka wananchi wa Handeni,
mkoani
Tanga kulitumia Tamasha la Handeni linalotarajiwa kufanyika Desemba 14
mjini hapa kwa ajili ya kutafuta fursa za kimaendeleo na kuwapatia
maisha bora Watanzania wote kwa kupitia sekta ya utamaduni.
Akizungumza
jana mjini Handeni, Muhingo alisema kutokana na tamasha hilo kufanyika mwisho
wa mwaka, Desemba 14, itakuwa chachu ya kuwaunganisha watu wote, sanjari na kujadili
changamoto zinazoikabiri Handeni na Tanzania kwa ujumla.
Muhingo alisema
kuwa tamasha hilo lina umuhimu mkubwa kutokana na kuandaliwa maalum kwa ajili
ya Watanzania kwa ajili ya kuangalia ngoma na matukio mbalimbali ya kijamii.
“Wakati
napongeza kwa dhati kuandaliwa kwa tamasha hili wilayani hapa, pia nawaomba
watu waje kwa wingi kushuhudia namna gani Handeni imepiga hatua kimaendeleo na
kuangalia namna gani wanaweza kusonga mbele.
“Naamini tutafikia
hatua nzuri kwa kushirikiana na wadau wote, hivyo wale wanaoishi mbali na
Handeni pia ni wakati wao kurudi nyumbani mwishoni mwa mwaka kujifunza mambo ya
utamaduni wao, sanjari na kufanya juhudi za kupiga hatua kimaendeleo,” alisema.
Tamasha hilo
linaloandaliwa na Mratibu wake Kambi Mbwana, hadi sasa limedhamiwa na Phed Trans, Clouds Media
Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah
Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.
Wengine ni duka la mavazi la Chichi
Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia
kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog,
Jiachie Blog na Taifa Letu.com, huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi hadi
saa 12 za jioni.
Mwisho
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :