JESHI LA POLISI KILIMANJARO LlNAMSHIKILIA KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 20 KWA KOSA LA KUMLAWITI MWENZAKE MWENYE UMRI WA MIAKA 16
Posted in
No comments
Tuesday, November 12, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Paul william, Moshi
Jeshi la
polisi mkoani Kilimanjaro limewakamata watu watatu kwa kosa la kufanya kitendo cha
kinyama cha kulawiti mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu katika shule ya
sekondari Nyerere iliyoko kijiji cha Lembeni wilayani Mwanga.
Akithibitisha
hayo kamanda wa polisi mkoani hapa Robart Boaz amesema tukio hilo lilitokea
Novemba 03 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni katika kijiji cha
Lembeni ambapo watuhumiwa hao walifanya kitendo hicho cha kinyama katika nyumba
inayomilikiwa na Charles Natanaeli alimaarufu Nguto.
Kamanda Boaz
amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Januari Alhaji(20) ambaye ni dereva wa magiri
ya fuso na Patriki Salpisi(20) ambaye ni fundi wa magari pamoja na mwenyenyumba
mwenyewe alimaarufu Nguto.
Amesema watuhumiwa
hao walitumwa kufanya kitendo hicho na mwalimu mmoja wa shule hiyo ya sekondari
Nyerere aliyetambulika kwa jina Hadija Juma.
Aidha Boaz
amesema hakuna taarifa zozote zilizoripotiwa polisi kuhusiana na kijana huyo
kutaka kufanya kitendo hicho na kuongeza
kuwa mwalimu huyo alituma vijana hao kufanya kitendo hicho kwa ajili ya
kulipiza kisasi ambapo inadaiwa huyo kijana alitaka kumbaka mtoto wa mwalimu
huyo mwenye umri wa miaka mitatu.
“Jeshi langu
la polisi halina taarifa zozote za kijana huyo kufanya kutaka kufanya kitendo
hicho nashangaa wao wanavyojitetea kwa kusema hivyo” alisema Boaz.
Hata hivyo
Boaz amemuagiza Mkuu wa polisi wilayani Mwanga kuhakikisha wanafuatilia kesi
hiyo kwa ukaribu ili kuhakikisha watuhumiwa hao wanapata adhabu kali
inayolingana na kosa hilo.
“Jeshi la
polisi litafuatilia kesi hiyo kwa ukaribu ili watuhumiwa hao wapate adhabu kali
na stahili na yeyote atakayewatetea na kuwaachia nitahakikisha ninapambana nae”
alisema Boaz.
Mwanafunzi
huyo alifikishwa katika hospitali ya Mwanga ambapo paka sasa yuko hapo kwa
ajili ya kuwekewa ukaribu wa washauri na saa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :