MAOFISA WAKAGUZI WASAIDIZI 810 WA JESHI LA POLISI NCHINI WAHITIMU MAFUNZO CCP JANA..
Posted in
No comments
Saturday, November 9, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Moshi
MAOFISA
810 wamehitimu mafunzo ya uafisa ukaguzi wasaidizi katika chuo cha Mafunzo ya
Jeshi la polisi Moshi (MPA) katika
mahafali yaliyofanyika jana katika viwanja vya chuo hicho na kuhudhuriwa na
Mkuu wa Jeshi hilo Nchini, IGP Siad Mwema.
Kuhitimu
kwa Maofisa wakaguzi hao 810 ambao wanaungana na wenzao 600 waliohitmu katika
mahafali ya Mwezi wa sita, kunafikisha idadi ya maofisa wakaguzi wa Jeshi hilo
kufikia 1410 kwa mwaka huu tu, ambapo kwa jumla hadi sasa jeshi la Polisi
nchini linajivunia kuwa zaidi ya Maofisa wakaguzi wapatao 10, 0913.
Akizungumza
na Wahitimu Hao pamoja na mamia ya Wananchi waliohudhuri sherehe za kufunga
mafunzo hayo yaliyodumu kwa takribani miezi sita Mahafali hayo, Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini, IGP-Said Mwema alisema Jeshi la Polisi nchini linapanga kuifanyia
maboresho sera ya Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi kwa kupeleka Maaskari wake
katika ngazi za Familia na Vijiji, mpango utakaojulikana kama mradi wa usalama
katikaFamilia.
IGP-Mwema |
IGP
Mwema alisema utafiti uliofanywa hivi karibuni na shikrika lisilo la serikali
la COSTEC kwa kushirikiana na Wanaharakati mbalimbali nchini pamoja na
wanafunzi wa chu kikuu cha Dar es salaam zinaonesha kuwa aslilimia 95 ya
wananchi wanakubali sera ya Polisi Jamii na ulinzi shririkishi katika ulinzi na
usalama wa Raia na mali yake.
Alisema
kuwa Jeshi lake limeanza mikakati ya kuhakikisha kuwa ulinzi unaimarika kwa
kuboresha sera ya polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa kupeleka mradi wa
usalama katika ngazi ya familia na kwa kuanzia, Maofisa wakaguzi wasaidizi
waliohitimu juzi watapelekwa katika Tarafa zote na vijiji kusadiana na serikali
za mitaa kulinda amani.
“Hii
ni hatua nzuri, kwa kulitambua hilo jeshi limepanga kuanzisha mradi wa usalama
katika ngazi ya familia na kwa kuanzia wahitimu 810 watapelekwa kusimamia mradi
huu,” alisema IGP Mwema.
Aidha
IGP Mwema aliongeza kuwa katika utekelezaji wa Mradi wa usalama katika ngazi ya
familia, Jkwa mwaka huu tu, Jeshi hilo limetenga maaskari zaidi ya 8000
watakaosambazwa nchi nzima.
Awali
akitoa ripoti za wahitimu hao kwa Mkuu wa Polisi nchini, IGP Said Mwema, Mkuu
wa chuo cha Mafunzo ya Polisi Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Matanga
Mbushi alisema Jumla ya Maofisa 813 walisajiliwa kujiunga na Mafunzo hayo, yaliyoanza
Machi 15, Mwaka huu.
ACP
Mbushi alisema kati ya hao 813 ni 810 tu ndio waliofanya mitihani na kufaulu
huku watatu wakishindwa kumalizia masomo yao akiwemo Askari mwenye namba F713
aliyefariki dunia baada ya kuugua ghafla, wa pili aliacha mwenyewe huku wa tatu
akiachishwa kutokana na sababu za kiafya.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :