KCMC YAIBUKA KINARA WA KULIPA KODI MKOANI KILIMANJARO
Posted in
No comments
Saturday, November 9, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na
Mwandishi wetu, Moshi
HOSPITALI
ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro (KCMC), imetangazwa kuwa mlipa kodi bora kwa
mwaka 2013 mkoani Kilimanjaro katika kitengo cha walipa kodi wakubwa wa mkoa
huo.
KCMC
imekuwaya kwanza kati ya Makampuni na Taasisi mbalimbali mkoani hapa
yaliyoshindanishwa katika kitengo cha walipa kodi wakubwa kutokana na juhudi
zake katika kuhakikisha inalipa kodi kutokana na huduma wanazotoa kwa jamii.
Hii
ni mara ya pili kwa Hospitali hiyo kuibuka wa Kwanza kwani mwaka 2011 KCMC
ilifanikiwa kupata tuzo ya mlipa kodi bora tuzo zinazotolewa kila mwaka na wakala
waKodi na makato nchini (TRA).
Akikabidhi
cheti cha ubora kwa Mkurugenzi wa Hospitali hiyo katika maadhimisho ya siku ya
mlipa kodi yaliyofanyika kimkoa jana katika viwanja vya Uhuru Hostel, ya mjini
Moshi, Meneja wa TRA mkoani Hapa, Patience Minga alisema kwa kuibuka mshindi wa kwanza kama
mlipa kodi mkubwa bora, Hospitali ya KCMC imedhihirisha kwamba inawajali wateja
wake.
Minga
alisema kuwa kila mwaka wamekuwa wakishindanisha makampuni na Taasisi
mbalimbali katika tuzo hizo kwa lengo la kuingeza ufanisi katika swala zima la
ulipaji kodi ikiwa ni pamoja na kuleta hamasa ya umuhimu wa kulipa kodi.
“Kila
mwaka, TRA tumekuwa tukishindanisha makampuni mbalimbali kwa lengo la kuongeza
hamasa katika swala la kulipa kodi ambapo pia huwa tunatoa elimu kwa wananchi
wote,” alisema Minga
Meneja
huyo alisema kuwa kila mwaka wamekuwa wakikusanya zaidi ya shilingi bilioni 10
mkoani Kilimanjaro kutokana na kodi huku akibainisha kuwa malengo yao kwa huu
ni kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 74.
Akizungumza
mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Rufaa ya KCMC, Prof. Moshi
Ntabaye alisema uongozi wa Hospitali hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na
serikali katika kuhakikisha inarudisha fadhila kwa jamii ya Tanzania ambayo
imeendelea kuiamini kwa takribani miaka 42 tangu ilipozinduliwa mwaka 1971,
katika huduma wanazotoa kwa kulipa kodi.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya rufaa ya KCMC Prof.Moshi Ntabaye akizungumza na wanahabari
baada ya kupata Hati na Tuzo ya ushindi kwa ulipaji bora wa kodi kwa Mkoa
wa Kilimanjaro kwa mwaka 2013.
|
Ntabaye
alisema ushindi huo unatokana na ukweli kwamba Hospitali ya KCMC imekuwa ikitoa
huduma bora ambayo inawawezesha kulipa kodi kwa wakati kila mwaka ambapo
alisema huwa wanalipa zaidi ya shilingi milioni mia moja kila mwaka.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo,
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dkt. Ibrahimu Msengi, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, aliwataka Wafanyabiashara na Wananchi kuendelea
kulipa kodi kila mara kwani nchi haiwezi kuendeeshwa bila kodi.
“Nchi yoyote ile haiwezi kuendeshwa bila Kodi, inatupasa
kulipa kodi kila mara bila shuruti, hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada
hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunalipa kodi ili uchumi wetu ukue,” alisema
Msengi.
Washindi wengine ni, Mfanyabishara Patrick Boisafi,
shule ya secondari ya St. Magreth, shule ya sekondari ya Kiraeni, Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADECO), shule ya sekondari ya international
Moshi pamoja na mengine mengi.
Mwisho.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :