MEYA WA KAMPALA AFURUMUSHWA OFISINI
Posted in
No comments
Monday, November 25, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Meya wa mji mkuu wa Uganda,
Kampala, ameondolewa ofisini na madiwani baada ya jopo maalum kumpata na
hatia ya matumizi mabaya ya mamlaka yake pamoja na kutokuwa na ujuzi wa
kutosha kwa kazi yake ambapo Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa Lukwago
Wafuasi wake wanaamini kuwa serikali ilipanga kumwondoa ofisini ili kuchukua wadhifa wa meya kutoka kwa upinzani.
Lukwago ni mwanachama wa chama cha upinzani cha Democratic Party (DP).Alichaguliwa kama meya mwezi Januari mwaka 2011.Wiki mbili zilizopita, serikali iliteua jopo lililomchunguza Lukwago na kuamua kuwa miongoni mwa makosa aliyoyafanya ni kukosa kuandaa mikutano muhimu , kupuuza wakuu waku wake na kuchochea umma kutolipa kodi.
Bwana Lukwago alitaja jopo hilo lililoongozwa na jaji kama, mahakama ya kipuuzi na kusema kuwa Rais Yoweri Museveni, ndiye aliyechochea jambo la kumwondoa ofisini ili washirika wake waweze kuchukua madaraka, baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2011.Vurugu zilizuka na kutatiza usafiri mjini Kampala baada ya wafuasi wa Bwana Lukwago kupinga kuondolewa kwake ofisini.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :