Posted in
By
danielmjema.blogspot.com
|
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiri (kulia), wakishuka
kutoka katika mv Songea, baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani
Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013.
|
|
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi, baada ya
kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya
akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. |
|
Nahodha wa mv Songea Tom Faya akimpatia maelekezo ya namna meli hiyo
inavyofanya kazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake,
wakati katibu mkuu huyo alipokuwa akisafiri na meli hiyo kutoka Mbamba
Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya, leo Nov 24, 2013. Kulia ni
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na
Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Kwenye usukukani ni Nahodha
Msaidizi, Conrad Shauritanga |
|
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison
Mwakyembe akimlaki wa furaha, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
alipompokea katibu mkuu huyo, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya
Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov
24, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. |
|
Baadhi ya abiria waliosafiri na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman
Kinana katika mv Songea, alipokuwa alitokea Mbamba Bay mkoani Ruvuma
kwenda Kyela mkoani Mbeya. Meli hiyo iliyoanza kazi katika Ziwa Nyasa,
mwaka 1974, ina uwezo wa kubeba abiria 213 wakiwemo wafanyakazi 13 wa
meli hiyo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).
|
0 MAOINI :