KIMENUKA!!! SIKU MOJA BAADA YA KIPIGO VIONGOZI YANGA WAAANZA KULUMBANA..

Posted in
No comments
Sunday, December 22, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

SIKU moja baada ya kupokea kichapo cha mbwa mwizi kutoka kwa Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Uongozi wa Simba umeanza kulumbana ambapo safari hii Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuph Manji amejikuta akilazimika kuingia katika Mzozo na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali, kuhusiana na uhallali wa Mlinda Mlango wake, anayedaiwa kuwa na Mapenzi na Klabu ya Simba, Juma Kaseja.

Manji, amesema tofauti na kauli tata za Mzee Akilimali Uongozi wa Yanga wanaamini, katika Usajili wao hawakumsajili Juma Kaseja ili waifunge Simba bali awasaidie katika michuano ya Afrika.


Manji ameyasema hayo leo asubuhi makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, siku moja baada ya Yanga kufungwa 3-1 na Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Kaseja akiwa langoni.

Manji alikuwa akimjibu Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali aliyeushutumu uongozi kusajili Juma Kaseja ni makosa. 

 “Huyu mzee nadhani umri umemzidi, lakini nataka nimkumbushe, huyo Ivo Mapunda aliondoka Yanga akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita na uongzi wa wakati huo kwa tuhuma za kufungisha kwenye mechi na Simba SC,”.

“Lakini pia nataka nimuulize, wakati Simba inarudisha mabao yote matatu Kaseja alikuwapo langoni? Nadhani hivi vitu si vizuri, tuache kulaumiana tushikamane kwa mustakabali mzuri wa timu,” alisema Manji.

Manji akionesha kukerwa na jambo uwanja wa Taifa

Manji amesema wanaheshimu uwezo wa Kaseja kwa sababu ndiye kipa aliyedaka mechi nyingi za mashindano ya Afrika kati ya makipa wote nchini, hivyo thamani yake haitashuka kwa kufungwa mabao matatu jana.
Ibrahim Akilimali


Pamoja na hayo, Manji amesema kwamba mechi ya jana haikuwa na uzito wowote kwao ni sawa na bonanza au fete, hivyo kufungwa haijawaumiza.

“Tuliamua kucheza kumfurahisha  mdhamini TBL, tumefungwa lakini bado tunaongoza ligi, hatujapoteza pointi hata moja, ile ilikuwa fete tu,”alisema Manji.

Manji amekiri Simba SC walicheza vizuri zaidi jana na walistahili ushindi na anawapongeza kwa hilo, pamoja na wadhamini, TBL kwa kuandaa mechi hiyo.

Manji amesema kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika wataboresha timu na benchi la ufundi na timu itaenda tena kambini Ulaya, hivyo anaamini mwakani makali yao yatafufuka na watatetea ubingwa.  

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .