MAWAZIRI WALIONG'OLEWA WAKACHA BUNGE
Posted in
No comments
Sunday, December 22, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
MAWAZIRI watatu kati ya wanne ambao Rais Jakaya Kikwete ametengua
uteuzi wao, jana walikacha kuhudhuria kikao cha Bunge kilichokuwa
kikifikia mwisho mjini Dodoma. Mawaziri hao, ambao hawakuonekana katika
viunga vya Bunge, ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel
Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha
na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.
Waziri pekee ambaye naye uteuzi wake ulitenguliwa aliyehudhuria kikao cha jana alikuwa ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David.Hata hivyo, Dk. Mathayo ndani ya ukumbi wa Bunge hakukaa katika kiti chake kilichoko upande wanaokaa mawaziri, badala yake alijichanganya katika viti vya wabunge nyuma kabisa ya Ukumbi wa Bunge.
Nchimbi na Nahodha, mbali na kutoonekana kabisa jana katika maeneo ya Bunge, tangu juzi waligoma kutoa maelezo yao bungeni kuhusu maoni ya Kamati na wabunge wakati walipoitwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda.Spika baada ya kuwaita mara kadhaa bila mafanikio, alisema amepata taarifa kwamba mawaziri hao watasemewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mawaziri hao kwa nyakati tofauti walitakiwa na Spika kutoa maelezo yao, lakini hata hivyo Nchimbi alitoka nje, na Nahodha, ambaye alikuwa amekaa viti vya nyuma hakusimama.Aliyekubali kuzungumza ni Kagasheki na Mathayo, ambapo Kagasheki alikiri kusikia maoni ya wabunge na kutangaza kujiuzulu.
“Mimi ni mtu mzima, nimesikia hisia nyingi za wabunge kwamba ni ‘take political responsibility’, Rais aliponiteua aliamini naweza kufanya vizuri, lakini kutokana na operesheni hii yametokea yaliyotokea,” alisema.
Kwa upande wake Dk. Mathayo, alijitetea kwamba hakuhusika katika operesheni hiyo na anashangaa amehusishwaje na mbaya zaidi Kamati haikumuita kumhoji.Alisema Wizara yake haihusiki na masuala ya kupima ardhi kwa ajili ya wafugaji na kwamba kama mipango na sera wizara yake inayo, ila inakwamishwa na ufinyu wa bajeti.
Jana wakati akihitimisha mkutano wa Bunge, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliwapongeza mawaziri waliokubali kuachia ngazi ili kulinda imani ya wananchi kwa serikali yao.Alisema hatua hiyo ni ya kuungwa mkono na kwamba Rais Jakaya Kikwete ameridhia kujiuzulu kwao.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru waheshimiwa mawaziri kwa ujasiri wao na kwa kutambua dhamana yao. Nawatakia kila la kheri katika shughuli zao za ubunge na nyingine kadri watakavyojaaliwa,” alisema Pinda.
Alisema Serikali itaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo ya Kamati ya Bunge na ya Bunge kwa ujumla kuhusiana na yaliyojitokeza katika Operesheni Tokomeza.Kwa upande wake, Spika aliwataka mawaziri kuwasimamia watendaji wao ili kuepusha matendo kama yaliyotokea katika operesheni hiyo na kusababisha mabadiliko ya mawaziri kila mwaka.
“Kila mwaka kamati hizi zinawasilisha taarifa zake bungeni, hatupendi kila mwaka mawaziri waondoke, mkiacha utaratibu huu kila mwaka watu wataondoka,” alisema.
Wakati huohuo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, alishauri kuundwa Tume ya uchunguzi ya kimahakama itakayoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa, ili kuchunguza matukio yote na kuwabaini wahusika wa vitendo hivyo viovu ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Waziri Mkuu alisema Rais ameridhia kuundwa kwa tume hiyo na amesema lazima ifanye kazi katika kipindi kifupi na kuleta taarifa yake haraka.

Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :