BAYERN NA ATHLETICO ZATINGA NUSU FAINALI, BARCELONA CHALI

Posted in
No comments
Thursday, April 14, 2016 By danielmjema.blogspot.com


Bayern
Bayern Munich imefuzu hatua ya nusu fainali ya Champions League kwa mara ya tano mfululizo baada ya kuitupa nje ya mashindano klabu ya Benfica ya Ureno.

Benfica ilikubali mkichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza ugenini, walifufua matumaini baada ya Raul Jimenez kupasia kamba kwenye mchezo wa marudiano wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani. Arturo Vidal alichomoa bao hilo kisha Thomas Muller kuongeza bao la pili na kuiweka mbele Bayern kwa magoli 2-1.



 Free-kick ya Talisca ilijaa moja kwa moja wavuni baada ya Javi Martinez kunusurka kulimwa kadi nyekundu kutokana na mchezo wake usio wa kiungwana. Bosi wa Bayern, Pep Guardiola ataungana na Manchester City msimu ujao na kuna uwezekano wa Droo itakayotolewa siku ya ijumaa ikaikutanisha Bayern na City katika hatua ya Nusu Fainali.

Boss wa Bayern Pep Guardiola atajiunga na Manchester City kipindi cha majira ya joto na klabu hizo mbili huenda zikakutana kwenye nusu fainali wakati draw ya kutafuta timu zitakazoumana kwenye hatua ya nusu fainali ya Champions League.

Takwimu muhimu;
  • Thomas Muller amefikisha magoli 36 kwenye michuano ya Champions League, magoli 10 zaidi ya mchezaji mwingine wa kijerumani.
  • Arturo Vidal anatarajia kushinda taji la ‘back-to-back’ kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu November 2013.
  • Benfica wamefunga magoli manne kwa vichwa kwenye Champions League, Bayern pekee ndiyo wanawazidi wakiwa wamefanya hivyo mara sita (6).
  • Bayern wamefika hatua ya nusu fainali ya Champions League mwa mara ya sita ndani ya misimu saba iliyopita.
  • Benfica wamefunga goli kwa free-kick ya moja kwa moja kwa mara ya kwanza tangu wafanye hivyo October 2011 (dhidi ya Basel).
Kwingineko, mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa Ulaya, FC Barcelona wamevuliwa ubingwa huo na Antoine Griezmann baada ya kuwashanga kwa kichapo cha magoli 2-0 kwenye mchezo wa marudiano wa robo fainali na kuikatia tiketi Atletico Madrid kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ya Ulaya.



Barcelona ilitua kwenye jiji la Madrid ikiwa mbele kwa magoli 2-1 kutoka kwenye mchezo wa awali lakini kutokana madhaifu ya safu yake ya ulinzi, wamejikuta wakiruhusu Griezmann kufanya yake kwenye uwanja wa nyumbani.

Barca walinyimwa penati dakika za lala salama baada ya Gabi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. Kichapo hicho kimefuta ndoto za Barca kutwaa mataji matatu (treble) ya La Liga, Champions League na Copa del Rey ndani ya msimu mmoja kama walivyofanya msimu uliopita huku wakiiacha Atletico kuungana na Bayern Munich, Manchester City na Real Madrid kufuzu kwa hatua ya nusu fainali. Draw ya kujua timu zipi zitapambana katika hatua ya nusu fainali itachezeshwa siku ya Ijumaa

Hstoria inajirudia

Mchezo huo ulikuwa ni wa nane kuzikutanisha Atletico Madrid na Barceolna ndani ya miezi 15, huku Barcelona ikiwa imeshinda michezo saba iliyopita. Hata hivyo usindi wa hivi karibuni wa Atletico dhidi ya Barcelona ulikuwa ni kwenye michuano ya Champions League kwenye hatua kama hii miaka miwili iliyopita.

Barcelona walitupwa nje ya michuano ya Ulaya kwa tofauti ya magoli 2-1 kwenye kichapo cha mwaka 2014 msimu ambao kikosi cha Diego Simeone kilifika hatua ya fainali na kupoteza mchezo mbele ya Real Madrid kwa bao 4-1 kwenye dakika 30 za nyongeza. 

Majanga yaendelea kumwandama Messi

Messi ameendelea kusalia kwenye rekodi yake ya kufunga magoli 499 kwenye maisha yake ya soka ambayo aliiweka tangu March 30 alipoifungia goli timu yake ya Argentina. Ameshacheza jumla ya dakika 452 bila kufuifungia goli klabu yake ya Barcelona.

Kwenye mchezo wa Jumatano, Messi hakuonekana kutaka kufunga kwasababu alishindwakupiga shuti hata moja lililolenga goli kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Champions League tangu mwaka 2014 ambapo ilikuwa dhidi ya Atletico.

Nyota huyo mwenye miaka 28 alikuwa chini ya uangalizi mkali wa Godin na Lucas Hernandez ambao walikuwa kwenye kiwango bora kwenye safu ya ulinzi ya Atletico.

Takwimu muhimu za mchezo;
  • Hakuna timu yeyote ambayo imewahi kutetea taji la Champions League tangu lilipopewa jina jipya msimu wa 1992/93.
  • Diego Costa pekee ndiye mchezaji wa Atletico Madrid aliyeweza kufunga magoli nane (8) kwenye michuano ya Champions League msimu wa 2013/14, Antoine Griezmann anaifukuzia rekodi hiyo akiwa ametupia kambani mara sita (6) hadi sasa.
  • Griezmann ameweza kufunga kwa mara nyingine tena kwenye michezo miwili dhidi ya timu moja, laifanya hivyo dhidi ya Galatasaray kabya ya Barcelona.
  • Barcelona wameshindwa kufunga goli kwenye mchezo wa Champions League kwa mara ya kwanza tangu April 2014 mchezo ambao pia ulikuwa ni dhidi ya Atletico Madrid.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .